Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wito wa Mungu kwa Ajili ya Matengenezo, Sura ya 110

    Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. Luka 1:17.Mar 118.1

    Kwa roho na nguvu ya Eliya, Yohana Mbatizaji alikwenda kuandaa njia ya Bwana na kugeuza watu kuelekea hekima ya wenye haki. Yeye alikuwa mwakilishi wa wale waishio katika siku hizi za mwisho ambao Mungu amewakabidhi kweli za kuwasilishwa kwa watu ili kuandaa njia kwa ajili ya kurudi kwa Kristo mara ya pili.Mar 118.2

    Wale wenye kuandaa njia kwa ajili ya kuja kwa mara ya pili kwa Kristo wanawakilishwa na Eliya mwaminifu, kama jinsi Yohana alivyokuja katika roho ya Eliya ili kutengeneza njia kwa ajili ya kuja kwa Kristo mara ya kwanza. Somo kuu la matengenezo linapaswa kuhamasishwa, na mawazo katika jamii yanapaswa kuamshwa. Kiasi katika mambo yote ni ukweli ambao unapaswa kuunganishwa na ujumbe, ili kugeuza watu toka katika ibada zao za sanamu, ulafi, na ubadhirifu unaoonekana katika mavazi na mambo mengine.Mar 118.3

    Kujikana nafsi, unyenyekevu, na kiasi vinavyohitajika kwa wenye haki, ambao Mungu anawaongoza na kuwabariki, ndivyo vinavyopaswa kuwasilishwa kwa watu dhidi ya ubadhirifu na mazoea yanayoharibu afya ya wale wanaoishi katika kizazi hiki kinachoshuka kimaadili. Mungu ameonesha ya kwamba matengenezo ya afya yapo katika muunganiko wa karibu sana na ujumbe wa malaika yule wa tatu kama jinsi mkono ulivyo karibu na mwili. Hakuna kitendo kilicho kikubwa kichopeleka kuharibika kimwili na kimaadili kama kilivyo kitendo cha kudharau fundisho hili. Wale wanaoendekeza tamaa ya kula na tamaa katika mambo mengine, huku wakifunga macho yao wasiione nuru kwa sababu ya hofu ya kuona mazoea ya dhambi ambayo hawapo tayari kuyaacha, wana hatia mbele za Mungu...Mar 118.4

    Watu wa Mungu wamekuwa wakiongozwa naye kutoka katika uzoefu wa mazoea ya kidunia, toka katika mazoea mabaya ya vyakula na tamaa zingine, ili wasimame katika jukwaa la kujikana nafsi na kiasi katika mambo yote. Watu wale ambao Mungu anawaongoza watakuwa wa pekee. Hawatakuwa kama dunia. Lakini kama watafuata uongozi wa Mungu watatimiza makusudi yake, na watakabidhi mapenzi yao kwa mapenzi Yake. Kristo ataishi ndani ya mioyo yao...”Mwili wako,“anasema mtume, “ni hekalu la Roho Mtakatifu.”Mar 118.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents