Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maonyo ya Mwisho ya Malaika Watatu, Sura ya 12

    Baada ya hapo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Ufunuo 18:1.Mar 20.1

    Malaika anayeungana na mwenziwe katika kutangaza ujumbe wa malaika yule wa tatu ataangazia dunia nzima kwa utukufu wake. Kazi ya ulimwengu mzima na uwezo usioelezeka imetabiriwa hapa. Msukumo wa kiadventista wa miaka ya 1840-44 ulikuwa ni udhihirisho wa uwezo wa Mungu; ujumbe wa malaika wa kwanza ulipelekwa kwa kila kituo cha kimishenari ulimwenguni, na katika baadhi ya nchi husika kukawa na shauku kubwa kuliko zote ambazo zilipata kuwepo katika nchi tangu nyakati za Matengenezo ya karne ya kumi na sita; lakini msukumo mkuu utakaokuja chini ya onyo la mwisho la malaika yule wa tatu utazidi misukumo yote iliyotangulia...Mar 20.2

    Kazi kuu ya injili itafungwa kwa udhihirisho wa uweza wa Mungu ulio mdogo kuliko ule ulioonekana wakati wa ufunguzi wake. Ule unabii uliotimizwa wakati wa kumwagwa kwa mvua ya awali litatimizwa tena wakati wa kilele cha mvua ya masika....Mar 20.3

    Watumishi wa Mungu, nyuso zao ziking’aa kutokana na kuwekwa wakfu, watakimbilia mahali mahali ili kuutangaza ujumbe wa mbinguni. Kutokana na sauti maelfu, onyo litatolewa dunia yote. Miujiza itatendeka, wagonjwa wataponywa, na ishara na maajabu vitawafuata waaminio. Ufu. 13:13. Kwa namna hiyo, wakazi wa dunia watafikishwa hatua ya kufanya maamuzi na kuyasimamia....Mar 20.4

    Machapisho mengi yaliyosambazwa na wamishenari yameweka mvuto wake, na bado wengi ambao mawazo yao yaliguswa yamezuiwa yasielewe: kweli kikamilifu au hata kukubali kutii. Sasa miali ya nuru inapenya kila mahali, kweli inaonekana katika uhalisia wake, na watoto wa Mungu walio waaminifu wanakata kamba ambazo zimekuwa zikiwashikilia. Miunganiko ya kifamilia, mahusiano ya kikanisa, haviwezi kuwazuia sasa. Kweli ni ya thamani kuliko mengine yote. Ijapokuwa kuna mawakala wengi walioungana kupinga kweli, bado idadi kubwa ya watu wanafanya maamuzi kusimama upande wa Bwana.Mar 20.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents