Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Dhana Potofu Kuhusu Mungu, Sura ya 125

    Kwa sababu, walipomjua Mungu hawamkutukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Warumi 1:21.Mar 133.1

    Dhana ya kwamba Mungu yumo katika viumbe vyote vya asili, ni moja ya mbinu tatanishi sana za Shetani. Inamwasilisha Mungu isivyo, na inaondoa heshima kwa ukuu na utukufu wake.Mar 133.2

    Mafundisho kuwa kila kiumbe ni mungu hayaungwi mkono na Neno la Mungu. Nuru ya kweli ya Mungu inaonesha kuwa nadharia hizi ni mawakala waangamizao roho. Msingi wake ni kiza na hisia za kibinadamu ndiyo eneo lake. Dhana hizi zinapendezesha moyo wa binadamu, na kuidhinisha uzorotaji wake. Kutengana na Mungu ni matokeo ya kuzikubali dhana hizi...Mar 133.3

    Ni mamlaka moja tu iwezayo kuvunja nguvu ya uovu toka mioyoni mwa watu, na hiyo ni nguvu ya Mungu iliyo ndani ya Yesu Kristo. Utakaso toka dhambini unapatikana tu kupitia kwa damu ya yule aliyesulubiwa. Neema yake pekee inatuwezesha kupinga na kushinda mielekeo ya asili yetu ya dhambi. Umizimu au dhana za mambo ya roho zinazohusianishwa na Mungu hufanya nguvu hii ya neema kukosa mguso. Kama Mungu ni nguvu iliyozagaa na kuwa ndani ya viumbe vyote, basi hilo linamaanisha kuwa yumo ndani ya watu wote; na ili mtu aweze kuupata utakatifu, basi anahitajika akuze tu uwezo ulio ndani yake.Mar 133.4

    Kama dhana hizi zikifuatiIiwa mantiki yake hadi kufikia hitimisho, zitaonekana dhahiri kuwa zinafutilia mbali utamaduni wa Kikristo, Zinaondolea mbali umuhimu wa upatanisho, na kumfanya mtu kuwa mwokozi wake mwenyewe. Dhana hizi kuhusu Mungu huzuia mguso wa Neno lake, na wale wanaozikubali wamo katika hatari kubwa ya kuongozwa hatimaye kufikia hatua ya kuiona Biblia kama inatokana na habari za kubuniwa tu. Hawa wanaweza kudai kupenda wema kuliko uovu; lakini Mungu anapoondolewa katika nafasi yake ya ukuu, wanaweka mategemeo yao katika nguvu ya kibinadamu, ambayo bila Mungu, haifai kitu. Nia ya mwanadamu isiposaidiwa haina uwezo wa kukataa na kushinda uovu. Ulinzi wa roho huvunjika. Mtu anakuwa hana kizuizi dhidi ya dhambi. Mara vizuizi vya Neno la Mungu na Roho wake vinapokataliwa, haiwezekani kujua mtu atazama katika kina cha upotofu kilicho kirefu kiasi gani.Mar 133.5

    Wale wanaoendelea kushikilia dhana hizi za ki-mizimu wataharibu maisha yao ya Kikristo, watakata muunganiko wao na Mungu, na kupoteza uzima wa milele.Mar 133.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents