Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    35 — Kutuliza Dhoruba

    Ilikuwa siku yenye shughuli nyingi siku hiyo. Kando ya bahari ya Galilaya, Yesu alikuwa amenena mfano wake wa kwanza, akieleza aina ya ufalme wake, na kusimamishwa kwake. Kazi yake aliifananisha na ile ya mpanzi wa mbegu. Maendeleo yake yakifanana na punje ya haradali, na pia matokeo ya chachu ndani ya unga. Mwisho wa kutengana baina ya wenye haki na waovu, aliwafananisha sawa na ngano na magugu, pamoja na juya la samaki. Fundisho muhimu pia alilifananisha sawa na hazina iliyositirika ndani ya shamba.TVV 183.1

    Wakati jioni ilipofika, makutano walikuwa bado yako pamoja naye, wakimsikiliza. Alikuwa amewahudumia kila siku bila kupata nafasi ya kula, na kupumzika. Na sasa jioni ilipofika alitafuta mahali pa faragha ili apumzike, maana alikuwa amechoka sana. Aliwaagiza wanafunzi wake wamfuate ng’ambo ya ziwa.TVV 183.2

    Baada ya kuwaaga makutano walimwingiza mashuani wakatweka. Lakini watu wengine, baadhi ya makutano, waliingia katika mashua ya kuvulia samaki iliyokuwa hapo pwani, wakamfuata, wakiwa na shauri ya. kumsikiliza.TVV 183.3

    Mwokozi akiwa amechoka na njaa pia, aliingia ndani ya mashua, chini akalala. Ziwa lilikuwa tulivu na bila upepo, lakini kwa ghafla mambo yalibadilika. Kukawa na giza, na mawingu, na tufani kubwa ikatokea, juu ya ziwa.TVV 183.4

    Mawimbi yalinguruma yakisukumwa na upepo mkali yakaingia ndani ya mashua, ikawa kivumbi. Hapo wavuvi mashujaa walipata taabu sana kukiongoza chombo chao. Juhudi yao haikufaulu. Wakakata tamaa ya kuokoa, maana waliona kuwa mashua yao inazidi kudidimia chini.TVV 183.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents