Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kwa nini Yuda alichukizwa

    Yuda hakuona kuwa kitendo hicho ni cha muhimu. Alianza kunung’unika, kwa kunong’onezea waliokuwa karibu naye, akimlaumu Yesu kwa kuruhusu kitendo hicho chenye hasara. Yuda aliyekuwa mtunza fedha wa wanafunzi alikuwa amechukua fedha kidogo kutoka katika akiba yao kwa matumizi yake binafsi, na kufanya mfuko wao kuwa hafifu. Alikuwa tayari kukusanya cho chote alichoweza kupata. Wakati akiona kuwa kitu fulani kikinunuliwa kisicho cha muhimu kwake, husema, kwa fedha hizo hazikuwekwa katika hazina yao aliyokuwa anaitunza ili kuwapa maskini?TVV 312.3

    Kitendo cha Mariamu kilitofautiana na kusudi lake la ubinafsi, kiasi kwamba aliaibika. Alitafuta kutoa sababu ya maana kwa ajili ya katazo lake kwa tunu hiyo; “Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?” Naye alisema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa kuwa ni mwivi” Laiti kama Marhamu ya Mariamu yangaliuzwa, na fedha kuwekwa mikononi mwake maskini wasingalipewa kitu.TVV 312.4

    Kwa kuwa Yuda alikuwa Bwana fedha alijidhani kuwa ni mkuu kuliko wanafunzi wenzake, na alikuwa na mvuto mkubwa sana kwao. Unafiki wake wa kuwapenda maskini uliwadanganya. Manung’uniko yalienea mezani yakisema: “Hasara yote hii ni ya nini? Marhamu hii ingaliuzwa na kuwagawia maskini.” Mariamu alisikia alivyoshutumiwa, naye katetemeka moyoni. Alidhani kuwa hata dada yake atamshutumu kwa hasara hii. Hata Bwana pia atamwona kuwa ni mfujaji wa vitu. Akuwa karibu kushusha moyo, wakati Bwana aliposikika akisema: “Mwacheni; mbona mnamtaabisha?” Yesu alijua kuwa katika kutenda hivyo alionyesha shukrani yake kwa ajili ya kusamehewa dhambi zake. Akipaza sauti yake, alisema: “Ametenda kazi njema; alivyoweza maana siku zote maskini mnao lakini mimi hamnami siku zote. Ametenda alivyoweza; ametangulia kupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.”TVV 313.1

    Manukato ambayo Mariamu angeipaka maridhawa maiti ya Mwokozi aliyapaka mwili wake ulio hai. Kwa kuipaka maiti, manukato hiyo ungepenya na kuenea pote kaburini lakini sasa ikafurahisha moyo wake Kristo. Kuonyesha upendo, wakati Mwokozi akingali hai ulikuwa uthibitisho wa kujitoa kwake, maana alikuwa ana mpaka mafuta kwa ajili ya maziko yake. Kristo alipoingia katika giza kuu la masumbuko yake, alikwenda na kumbukumbu ya kitendo hicho cha upendo na uaminifu ambao utakuwa wake kutoka kwa watakaookolewa milele na milele.TVV 313.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents