Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    70 — Kristo Ashirikiana na Wenye Dhiki na Masikini

    “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu . . . ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua. Hivyo ndivyo Kristo alivyoelezea picha ya siku kuu ya hukumu itakavyokuwa. Wakati mataifa yatakapo-kusanyika mbele zake, kutakuwapo na makundi mawili tu, na mwisho wao, utaamuliwa kutokana na yale ambayo walimtendea, au yale ambayo hawakumte-ndea, kwa njia ya kuwahudumia maskini na wenye dhiki.TVV 360.1

    Katika siku hiyo Kristo hatatoa mbele za watu kazi kuu aliyowatendea kwa kutoa uhai wake kwa ajili yao, ila ataweka hadharani kazi waliyomtumikia kwa uaminifu. Atasema: “Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.” Lakini wanaosifiwa hivyo na Kristo hawajui kuwa walimhudumia. Kwa maswali ya mshangao wao Anawajibu, “kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”TVV 360.2

    Yesu alisema: Katika wale wote wanaoudhiwa kwa ajili ya jina langu, mnapaswa kunitambua humo. Na kadiri ambavyo mgenihudumia, ndivyo mwahudumie wao. Wale wote waliozaliwa katika jamaa ya mbingu kwa namna maalum ni ndugu za Bwana wetu. Upendo wa Kristo huwafunga pamoja jamaa wote wa familia yake. “Na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.” 1 Yohana 4:7.TVV 360.3

    Wale wanaosifiwa na Kristo katika siku ya hukumu, inawezekana kuwa walikuwa Wanajua theolojia kidogo tu, lakini walizipenda kanuni za mbinguni. Hata miongoni mwa watu wasioamini wako wenye moyo wa ukarimu. Kabla maneno ya uzima hayajaingia katika masikio yao waliwafadhili wahubiri bila kujali hatari zilizowakabili. Wanaomwabudu Mungu bila kujua, ambao hawajapata nuru yo yote ile hawatapotea. Ingawa hawaijui sheria ya Mungu iliyoandikwa, wamefanya mambo yanayotakiwa na sheria. Matendo yao hudhihirisha kuwa Roho Mtakatifu ameyagusa maisha yao; nao wanatambuliwa kuwa ni wana wa Mungu.TVV 360.4

    Kutakuwa na mshangao kiasi gani kwa watu wanyonge kusikia, wakiambiwa na Mwokozi: “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”!TVV 361.1

    Lakini upendo wa Kristo hauna mpaka kwa watu wa kundi lo lote lile. Yeye ni Mwana wa Adamu, hivyo ndugu wa kila mwana na binti wa Adamu. Wafuasi wake wasijione kuwa wametengwa na ulimwengu uwazungukao na unaoangamia. Waoni sehemu ya utandu wajamaa kuu ya wanadamu, ni ndugu zao wenye dhambi na wenye haki pia. Upendo wa Kristo huwakumbatia wenye dhambi na walioangukia mbali; na kila kitendo kinachofanywa ili kumwinua mkosaji kutoka matopeni, hukubaliwa kana kwamba kimetendwa kwa Kristo.TVV 361.2

    Malaika wa mbinguni hutumwa ili kuwahudumia wale watakaourithi wokovu. Haijadhihirika bado kwamba ni nani watakaourithi wokovu, lakini malaika wanazungukazunguka duniani kote wakitafuta kuwafariji wenye huzuni na kuwalinda walio hatarini na kuwaleta watu kwa Kristo. Hakuna hata mmoja anayepitwa. Mungu hana upendeleo.TVV 361.3

    Unapofungua mlango wako kwa wenye dhiki na wasumbukao, unawakaribisha malaika wasioonekana. Huleta utulivu na furaha. Kila tendo la huruma hupeleka wimbo mzuri mbinguni. Baba katika kiti cha enzi huwahesabu wenye matendo yasiyo na ubinafsi kuwa hazina yake ya thamani kuu.TVV 361.4

    Wale watakaokuwa katika mkono wa kushoto wa Kristo, ambao hawakumshughulikia yeye katika wenye dhiki, ambao ni maskini na wenye dhiki, hawakutambua hatia yao. Waliishi katika hali ya ubinafsi wala hawakujali haja za wengine,TVV 361.5

    Mungu amewapa matajiri mali ili wawasaidie wenye dhiki ambao ni watoto wake, lakini mara nyingi hawajali dhiki na mahitaji ya watu wengine. Hawaelewi majaribu na matatizo ya maskini, na hivyo huruma hufifia katika mioyo yao. Mali waliyopewa na Mungu, ili wawasaidie wenye dhiki, wao huzitumia katika majivuno na ubinafsi wao. Maskini hunyimwa maarifa wanayopaswa kupata kuhusu huruma za Mungu, kwa sababu amefanya kila mpango ili wasaidiwe kwa kupatiwa mahitaji, ya lazima. Huachwa kusumbuka na ufinyu wa maisha ya umaskini na kuingia katika majaribu ya wivu na kujazwa na dhana Potovu.TVV 361.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents