Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    71 — Mtumishi wa Watumishi

    Kristo pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamekusanyika pamoja ili kuadhimisha Pasaka. Mwokozi alijua kuwa saa yake imekuja; Yeye mwenyewe alikuwa ndiye Mwana Kondoo wa kweli wa pasaka, na katika siku ile ya kula Pasaka, ilikuwa budi atolewe kafara. Kulikuwa na saa chache ambazo atazitumia kwa manufaa ya wanafunzi wake.TVV 364.1

    Maisha ya Kristo yalikuwa ya huduma isiyokuwa na ubinafsi ndani yake. “Kama vile Mwana Adamu asivyokuja kutumikiwa bali kutumika,” (Mathayo 20:28), hilo lilikuwa fundisho katika kila tendo lake. Lakini wanafunzi wake walikuwa hawajajifunza fundisho hilo bado. Wakati wa Pasaka hii ya mwisho Yesu alihangaika. Kivuli cha kilimtanda usoni. Wanafunzi walitambua kuwa kulikuwa na jambo zito lilomsumbua sana.TVV 364.2

    Walipokuwa wamekusanyika mezani, akawambia; “Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi, maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.” Luka 22:15-18.TVV 364.3

    Sasa Kristo alikuwa katika kivuli cha msalaba, na maumivu ya uchungu yalisonga rohoni mwake. Alijua kuwa ataachwa; alijua kuwa kwa hali ya kudhalalisha mno atahukumiwa kuuawa kama mhalifu. Alijua kutokuwa na shukrani na ukatili, wa wale aliokuja kuwaokoa. Alijua kuwa kwa wengi dhabihu atakayowafanyia haitathaminiwa. Akijua yote yaliyokuwa yako mbele yake, katika hali ya kibinadanu angaliweza kulemewa, na mawazo ya kudhalilishwa na mateso yake. Lakini hakujifikiria mwenyewe. Bali kuwafikiria wanafunzi wake ndiko kulikokuwa katika moyo wake.TVV 364.4

    Katika jioni hii ya mwisho, Yesu alikuwa na mambo mengi ya kuwaambia wanafunzi wake. Lakini aliona kuwa hawangeweza kustahimili yote. Alipowaangalia, usoni, maneno yake yalibaki mdomoni. Wakati ulipita kimya kimya. Wanafunzi walikuwa wenye mashaka makubwa. Walivyokuwa wakitazamana ilionyesha hali ya mashindano na wivu.TVV 365.1

    Kulikuwa na “mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa.” Mabishano haya yalimuumiza na kumhuzunisha Yesu. Kila mmoja aliwania nafasi ya juu katika ufalme. Kule kuthubutu kwa Yakobo na Yohana kuitaka nafasi ya juu kuliwajongeza wale kumi kiasi cha kutaka kuleta kufarakana. Yuda ndiye alikuwa mkali sana dhidi ya Yakobo na Yohana.TVV 365.2

    Wanafunzi walipoingia chumba cha juu, Yuda alimsogelea Kristo upande wa mkono wa kushoto, Yohana alikuwa mkono wa kulia. Kama kulikuwa na cheo cho chote cha juu Yuda alikusudia kukipata.TVV 365.3

    Jambo jingine la ubishi lilikuwa limetokea. Ilikuwa kawaida kwa mtumishi kuwaosha miguu wageni. Katika siku hii, mtungi wa maji ulikuwako, chombo cha kunawia, na kitambaa cha kufutia, vyote vilikuwa tayari; lakini mtumishi wa kuhudumu hakuwako kwa hiyo ilikuwa kazi ya wanafunzi kufanya huduma hiyo. Lakini kila mmoja hakutaka kufanya kazi hiyo inayompasa mtumishi. Wote walionyesha hali ya kutojali huduma hiyo. Kukaa kimya kwao kulionyesha kutonyenyekea.TVV 365.4

    Ni jinsi gani Kristo atawasaidia maskini hawa ili Shetani asiweze kupata ushindi kamili dhidi yao? Atawasaidiaje wajue kuwa kule tu kujidai kwamba ni wanafunzi hakuwafanyi kuwa wanafunzi wa kweli? Atawaamshiaje upendo katika mioyo yao kuwawezesha kutambua kile alichotamani kuwaaambia?TVV 365.5

    Yesu alingoja kidogo aone watakaofanya nini. Kisha yeye ambaye ni Mwalimu wa mbinguni, aliondoka mezani. Akivua mavazi yake ya juu, alichukua kitambaa cha kufutia. Wanafunzi wakiwa kimya walingoja kuona yatakayofuata. “Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.” Tendo hilo liliwafungua macho wanafunzi. Aibu kuu ikawajaza mioyo na wakajiona katika nuru mpya.TVV 365.6

    Kristo aliwapa kielelezo ambacho hawangekisahau kamwe. Upendo wake kwao ulikuwa usioweza kuvunjika kirahisi. Alikuwa na ufahamu hakika wa Uungu wake; lakini aliweka kando taji yake ya ufalme, na akatwaa hali ya mtumwa. Mmojawapo ya matendo yake ya mwisho ya maisha yake hapa duniani lilikuwa kujifunga kama mtumwa na kutenda kazi ya mtumwa.TVV 365.7

    Kabla ya Pasaka Yuda alikuwa amekamilisha njama na makuhani na waandishi, ya kumkabidhi Yesu katika mikono yao. Wanafunzi hawakufahamu lo lote kuhusu makusudi ya Yuda. Yesu peke yake ndiye aliyefahamu siri yake, walakini Yesu hakumuumbua Yuda kwa wanafunzi. Alijisikia kuwa na mzigo na Yuda kama alivyousikitikia Yerusalemu na kuulilia mji uliokuwa unakabiliwa na maafa.TVV 366.1

    Nguvu ya msukumo wa upendo wa Kristo ulimgusa Yuda. Wakati mikono ya Mwokozi ilipomshika miguu na kumtawadha, moyo wake ulisisimka, Yuda akajisikia kuungama dhambi yake. Lakini hakutaka kunyenyekea. Akafanya moyo wake kuwa mgumu dhidi ya toba na kwa mara nyingine tena misukumo ya zamani ikamtawala. Yuda sasa akachukizwa na tendo la Yesu la kuwatawadha miguu wanafunzi wake. Alifikiri kwamba, ikiwa Yesu anajidhili kiasi hicho asingeweza kuwa mfalme wa Israeli. Alipoona hivyo akaridhika kuwa hakukuwa na la manufaa kumfuata Kristo. Alithibitika katika kusudi lake la kumkana Kristo na kuamini amedanganyika. Akiwa amepagawa na pepo mbaya, aliazimia kutekeleza kazi aliyokuwa amekubali kutenda katika kumsaliti Bwana wake.TVV 366.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents