Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kutenda Kinyume cha Kristo

    Yuda alikuwa akiendeleza wazo kwamba Kristo atatawala kama mfalme katika Yerusalemu. Wakati Kristo alipofanya muujiza wa kulisha watu kwa mikate Yuda alikuwa mstari wa mbele katika watu waliotaka kumtawaza Yesu kwa lazima. Matumaini yake yalikuwa makubwa sana, kutokufanikiwa kwake kukawa uchungu. Mazungumzo ya Kristo kuhusu mkate wa uzima, yalikuwa ndiyo kikomo. Alimwona Kristo akielekea katika mambo ya kiroho zaidi kuliko mambo ya kidunia. alidhani kuwa Kristo hakutaka heshima, na wala hakukusudia kuwakuza wafuasi wake. Aliazimu kutoshirikiana sana na Kristo na badala yake kujitenga polepole. Basi aliamua kuwa mtazamaji na hasa alikuwa mtazamaji.TVV 404.3

    Tangu wakati huo alionyesha mashaka yaliyowachanganya wenzake. Alileta mabishano na mafungu ya Biblia juu ya mambo ambayo hayakuwa na uhusiano na yale yaliyofundishwa na Kristo. Mafungu ya Biblia hayo yaliwachanganya wanafunzi wa Yesu na kuzidisha kufa moyo kwao kwa sababu yalinyofolewa kutoka katika maana yake. Walakini Yuda alijionyesha kuwa mwaminifu. Hivyo kwa njia ya kuonekana mwenye dini na busara alikuwa anayahusisha na maana ambayo haikukusudiwa na Yesu. Mapendekezo yake yalikuwa yanasisimua na kuongeza msukumo wa kupendelea mambo ya ulimwengu. Mawazo ya nani atakuwa mkuu kwa kawaida yalisisimuliwa na Yuda.TVV 404.4

    Wakati Yesu alipomwambia yule kijana, mtawala tajiri masharti ya kuwa mwanafunzi. Yuda alidhani kuwa kosa limetendeka. Watu kama mkuu huyu wangesaidia kuendeleza kazi ya Kristo. Yuda alifikiri kuwa yeye binafsi angebuni njia nzuri za kusaidia kanisa dogo hili kufanikiwa. Katika mambo hayo alijidhania kuwa ana hekima kuliko Yesu.TVV 405.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents