Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wengi Walifufuka Pamoja na Yesu

    Jinsi Kristo alivyofufuka, aliwaleta wengi wa wafungwa waliolala. (Tazama Mathayo 27:52.) Ni wale walioshuhudia ukweli mpaka wakatoa maisha yao. Sasa watamshuhudia aliyewafufua kutoka katika wafu.TVV 443.4

    Wakati wa huduma yake, Yesu alikuwa amefufua wafu. Lakini hawa waliofufuliwa hawakuvikwa hali ya kutokufa. Lakini wale waliofufuka wakati wa kufufuka kwa Yesu, walivikwa hali ya kutokufa milele. Walipanda pamoja na Yesu kama nyara wa ushindi wake dhidi ya mauti na kaburi. Waliingia mjini, wakawatokea wengi, wakitangaza kwamba Kristo amefufuka, kutoka kwa wafu nao wamefufuka pamoja naye. Watakatifu waliofufuka walishuhudia ukweli wa maneno; “Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka.” Isaya 26:19.TVV 443.5

    Katika Mwokozi wetu, uzima uliopotea kwa sababu ya dhambi, unarudishwa. Alipewa uwezo wa kuwapa watu hali ya kutokufa. Asema: “Mimi Nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Yohana 10:10. “Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.” Yohana 6:54. Kwa mkristo kifo ni kulala usingizi wakati wa ukimya na giza. “Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.” Wakolosai 3:4.TVV 444.1

    Sauti iliyopazwa msalabani, “Imekwisha”, itapenyeza makaburi na kuyabomoa, na wafu waliokufa katika Kristo watafufuka. Wakati Kristo alipofufuka makaburi machache yalifunguliwa, lakini wakati wa kuja kwake mara ya pili, watu wake wote walio wateule, watasikia sauti yake, nao watatoka, wakiwa na hali ya utukufu ya kutokufa. Uwezo ule ule uliomwamsha Kristo kutoka kwa wafu utaliinua kanisa lake juu ya nguvu zote, siyo katika dunia hii, bali pia katika ulimwengu ujao.TVV 444.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents