Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Shetani huduma kuwa Adui Aliyeshindwa.

    Mwishoni Shetani alitambua kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Uungu ulipita katika ubinadamu. Shetani alipaswa kuondoka mbele yake, ambaye ni Mkombozi wa ulimwengu. Ushindi wa Yesu ulikuwa kamili, kama kushindwa kwa Adamu kulivyokuwa kamili.TVV 64.4

    Vivyo hivyo na sisi twapaswa kuyapinga majaribu, na kumdhalilisha Shetani atuache. Yesu alipata ushindi kwa njia ya utii kwa sheria ya Mungu, na imani imara kwa Mungu. Naye asema kwetu kwa njia ya mtume: ‘Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atakimbia. Mkaribisheni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” Yakobo 4:7, 8. “Jina la Bwana ni mnara imara. Mwenye haki huukimbilia, akawa salama.” Mithali 10:10. Shetani hutetema wakati mtu dhaifu anapokimbilia kwenye jina hilo imara.TVV 64.5

    “Shetani alipoondo kwa Yesu, Yesu alianguka ameishiwa na nguvu zote, akiwa karibu kufa. Malaika walikuwa wakimtazama jemadari wao, alipokuwa akishindana na majaribu, ambayo ni makali mno, sisi hatuwezi kuyakabili. Sasa walimhudumia Mwana wa Mungu, alipokuwa akilala kama mtu anayekufa. Alitiwa nguvu na Mungu, akifarijiwa kuwa mbingu yote inashangilia ushindi wake. Alipozindukana tena, roho yake ikawaka kwa upendo, jinsi alivyowapenda watu; akaendelea kukamilisha kazi aliyokuja kuifanya, ambayo sasa ameianza, naye hatapumzika mpaka taifa la wanadamu limekombolewa.TVV 65.1

    Gharama ya ukombozi haitatambulikana kamwe, mpaka wakati waliokombolewa watakaposimama na Mwokozi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ndipo utukufu wa makao ya milele utakapofunuliwa katika akili zetu, na kushangaa kwa furaha, tutakumbuka ya kwamba Yesu aliacha yote kwa ajili yetu, na kwamba, kwa ajili yetu alijihatarisha hivyo kuwaokoa waliopotea milele, hapo tutapaza sauti tukiimba: “Anayestahili sifa na shukrani ni MwanaKondoo, aliyechinjwa, ndiye astahiliye kupokea uwezo, na utajiri, na hekima, na nguvu na heshima, na utukufu, na mibaraka.” Ufunuo 5:12.TVV 65.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents