Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mwanzo wa Kumkataa Kabisa Kristo

    Makuhani na wakuu, wangalimwona Yesu kuwa ni mpakwa mafuta wa Mungu, maana walikuwa na maandiko ya unabii uliokuwa ukiieleza kazi ya Kristo. Walijua kuwa kutakaswa kwa hekalu kulifanywa kwa uwezo unaozidi wa kibinadamu. Ijapokuwa walimchukia Yesu, wasingalikimbia, isipokuwa walikuwa na wazo kuwa, labda ni nabii aliyetumwa na Mungu ili kulitakasa hekalu. Wakiwa na wazo la jinsi hiyo walimwendea na neno, kwamba, “Unatuonyesha ishara gani kwamba unafanya mambo haya?”TVV 85.4

    Yesu alikuwa amewaonyesha ishara. Katika kufanya kazi ambayo Masihi atakuja kufanya, alikuwa amewaonyesha tabia yake jinsi ilivyo. Sasa aliwajibu kwa mfano, akiwaonyesha kuwa anasoma mawazo yao, ambayo ni mabaya. Alisema: “Livunjeni hekalu hili, nami nitalilenga kwa muda wa siku tatu.”TVV 85.5

    Kwa kusema hivyo hakumaanisha kujivunia hekalu la Wayahudi na ibada yao, bali kwa kifo chake, yaani kulivunja hekalu la mwili wake. Jambo hili la kumwua Wayahudi walikuwa wamelilia njama. Wakati makuhani na wakuu waliporudi hekaluni, walikuwa wamekusudia kumwua Yesu ili kuondoa ghasia. Walakini waliyachukua maneno yake, kana kwamba yalihusu kuvunja hekalu lililokuwa Yerusalemu. Na kwa chuki walisema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita, nawe utalijenga kwa siku tatu tu?” Sasa waliona kuwa Yesu ameitia kasoro imani yao, kwa hiyo walithibitisha msimamo wao wa kumkataa.TVV 85.6

    Kristo alijua kuwa maneno yake yangaliwakera vibaya, na kumdhania vingine. Wakati wa mashitaka yake ya mwisho, katika kusulibishwa kwake, wangalimtupia maneno hayo. Lakini kuyafafanua wakati huu kungewajulisha wanafunzi wake juu ya mateso yatakayompata, na kungeleta huzuni kubwa na kusononeka. Wakati huu hawajawa tayari kupokea mambo kama hayo. Kuyafafanua mambo hayo, kungefanya Wayahudi wafunike unafiki wao na kujifanya kuwa waaminifu kabisa. Maana wamekwisha kukanyaga katika njia itakayowaongoza kwenye mwisho wa kumchinja Yesu kama Mwana Kondoo apelekwaye machinjioni.TVV 86.1

    Kristo alijua kuwa maneno haya yatakaririwa. Ingawa yamesemwa kwa watu wachache katika pasaka, yatachukuliwa na kutangazwa kwa watu maelfu ulimwenguni. Baada ya kufutuka kwake kutoka ufuni, maneno haya yatafahamika wazi. Kwa wengi wao yatakuwa ni ushahidi wa Uungu wake, uliofichika.TVV 86.2

    Maneno ya Mwokozi kwamba: “Livunjeni hekalu hili nami nitalisimamisha kwa siku tatu, yalikuwa na maana kubwa sana, kiasi cha kukaririwa na wasikilizaji wake. Huduma za hekaluni zilikuwa mfano wa dhabihu ya Mwana wa Mungu. Mpango mzima wa matoleo ya kafara na huduma zake, ulikuwa unaelekeza juu ya kifo cha Mwokozi cha kuwaokoa wakosaji. Kanuni ya uwekevu wa mali haukuwa na faida yoyote mbali na yeye. Wakati Wayahudi walipobadilisha kusudi lao la kumkataa Yesu, na kumtoa ili auawe, walikataa mambo yote ya utulivu hekaluni pamoja na huduma zake. Utakatifu ndio ulioondokana nao. Sasa walipaswa kuangamizwa. Tangu siku hiyo dhabihu zote zilizokuwa zikitolewa hazikuwa na maana yoyote. Katika kumwua Kristo, kwa kweli Wayahudi walilivunja hekalu. Kristo aliposubishwa pazia la hekalu lilipasuka vipande viwili toka juu mpaka chini kuonyesha kuwa dhabihu halisi iliyo ya mwisho imetolewa. Kawaida ya kutoa dhabihu za wanyama, ilikoma kabisa.TVV 86.3

    “Nitalisimamisha kwa siku tatu.” Kutoka katika kaburi la Yusufu lililopasuka, Yesu alitoka akiwa mshindi hasa. Kwa kilo chake na kufufuka, Kristo alikuwa “mhudumu wa hema ya kweli, ambayo Bwana ndiye mjenzi wake, wala si mwanadamu.” Wagalatia 8:2. Watu walisimarnisha hema au hekalu la Wayahudi, lakini hekalu la juu, halikujengwa na fundi wa kibinadamu. “Mtu ambaye jina lake ni Chipukizi . . . atalijenga hekalu la bwana . . . naye atauchukua huo utukufu, naye ataketi na kutawala katika kiti cha enzi.” Zekaria 6:12, 13.TVV 86.4

    Huduma ya dhabihu ambayo ilikuwa ikimwonyesha Kristo ilipita. Lakini macho ya watu yaligeukia dhabihu halisi ambayo ni dhabihu ya dhambi ya ulimwengu. Makuhani na ukuhani ulikoma, lakini tunamwangalia Yesu mhudumu wa agano mpya. “Njia iendayo katika utakatifu ilikuwa haijadhihirika, wakati hema ya kwanza ilipokuwa ingalipo . . . lakini Kristo ajapo yeye aliye kuhani mkuu wa mambo mema yajayo, ni hudumu bora katika hema bora zaidi isiyofanywa kwa mikono, bali kwa damu yake mwenyewe, aliingia mara moja katika patakatifu, akafanya ukombozi kwa ajili yetu.’ Waebrania 9:1-12.TVV 87.1

    “Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye, maana yu hai siku zote ili awaokoe.” Waebrania 7:25. Ingawa hekalu la mbinguni na kuhani wetu mkuu huonekana wazi, wanafunzi hawangeona kuwa kuna mavunjiko kati yao na mbingu, na hakuna uwezo walio nao kwa ukosefu wa kuwako kwa Yesu kati yao. Yesu alipojidhihirisha hekaluni mbinguni, huendelea kwa Roho yake, kujionyesha katika kanisa lake duniani. Neno lake la kuagia watu wake lilitimia, “Tazama, mimi niko pamoja nanyi siku zote, mpaka mwisho wa dunia. Mathayo 2:20TVV 87.2

    “Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana nasi katika mambo yetu ya udhaifu, bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. Waebrania 4:15, 16.TVV 87.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents