Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Moyo wa Mama Anyonyeshaye

    Chakula bora kabisa kwa mtoto mchanga ni chakula kile ambacho hupatikana kutoka mwilini. Si vizuri kumnyima mtoto chakula hiki bila sababu ya kutosha. Ni ukatili mama, kwa ajili ya kujitakia nafasi au starehe, kujaribu kuepukana na kazi hii ya kumnyonyessha mtoto wake mdogo.KN 159.6

    Wakati ambapo mtoto mchanga kunyonya ziwa la mama ni wa shida. Mama wengi, wakiwa wananyonyesha watoto wao wachanga, wameachwa kutumika kupita kiasi na kutia joto damu yao kwa kupika chakula; mtoto mchanga amepatwa na madhara vibaya, siyo tu kushindwa na homa inayotokana na kunyonya ziwa la mamaye, bali hata damu yake imetiwa sumu kwa chakula kisicho kizuri kwa afya cha mama, ambacho huutia homa mwili wake mzima, na kukidhuru chakula cha mtoto. Vile vile mtoto atapata madhara kwa hali ya moyoni mwa mama. Kama hana furaha, mwepesi kufadhaika, mwenye kukasirika upesi, mwenye kupandwa na hasira upesi, ziwa anyonyalo mtoto kutoka kwa mamaye litawaka, na mara nyingi, hali italeta msokoto wa tumbo, mpindano, na mara zingine kujipindapinda kwa ugonjwa, na ugonjwa wa ghafula wa muda.KN 160.1

    Kadhalika tabia ya mtoto husaidiwa au kudhuriwa na chakula apatacho kutoka kwa mama. Basi, ni jambo kubwa kama nini kwamba mama, wakati anyonyeshapo, angekuwa na moyo wa furaha, akijitawala kabisa moyoni mwake mwenyewe. Kwa kufanya hivi, chakula cha mtoto hakitapata madhara yo yote, na mwenendo mtulivu wa kujiweza nafsi ambao mama huufuata katika kumtendea mtoto wake huhusiana sana na kule kuyafanyiza mawazo ya moyoni mwa mtoto mchanga. Kama akiwa mwepesi wa hasira, tabia ya uangalifu, na saburi ya mama itakuwa na mvuto wa kumtuliza mtoto na kumsahihisha, na afya ya mtoto yaweza kupata nafuu kubwa.KN 160.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents