Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Haja ya Kujizuia Katika Kumtawala (Kumwadhibu) Mtoto

    Katika malezi ya mtoto pana nyakati ambapo nia thabiti, ya utu uzima, ya mama inapokutana na nia kaidi, siyo ya haki, ya mtoto. Nyakati kama hizo inatakikana busara kubwa upande wa mama. Kwa kutotumia busara, kushurutisha kwa ukali, madhara makubwa huweza kufanywa kwa mtoto.KN 161.2

    Kila iwezekanapo, matata haya yangeepukwa; maana huleta mashindano makali kwa mama na mtoto. Lakini mara matata ya namna hii yatukiapo, hubidi nia ya mtoto kushindwa na nia ya akili zaidi ya mzazi.KN 161.3

    Yampasa mama kujizuia kabisa, asifanye jambo lo lote litakaloamsna ndani ya mtoto moyo wa kuasi amri (kutaka shari). Asitoe amri kwa sauti kubwa. Atafaidiwa zaidi akisema kwa sauti ndogo ya upole. Yampasa, kumtendea mtoto kwa njia itakayomvuta kwa Yesu. Anapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Msaidizi wake; upendo ndio uwezo wake.KN 161.4

    Kama yu Mkristo mwenye busara hatathubutu kumshurutisha mtoto kutii. Humwomba Mungu kwa bidii ili adui asipate kushinda, na, akisali hufahamu nafsim kufanywa upya maisha ya kiroho. Huona kwamba uwezo ule ule utendao kazi ndani yake hutenda kazi ndani ya mtoto pia. Huwa mpole zaidi. Ushindi umepatikana. Uvumilivu wake, wema wake, maneno yake ya hekima na kiasi, yamefanya kazi yao, Kuna amani baada ya matata, kama mwangaza wa jua bada ya mvua. Nao malaika, ambao wameyatazama mambo hayo, huimba mara hiyo nyimbo za furaha.KN 161.5

    Matata ya namna hii huingia pia katika maisha ya mume na mke, ambao, isipokuwa wanatawaliwa na Roho wa Mungu, nyakati kama hizo wataonyesha moyo wa ghadhabu ya ghafula usio wa akila ambao unaonyeshwa mara nyingi na watoto. Jiwe gumu likipiga jiwe lingine gumu kutakuwako na ushindani wa nia moja kushindana na nia nyingine. 37747, 48.KN 162.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents