Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uwezo wa Mama kwa Mema

    Pengine hali ya mama ni duni; lakini mvuto wake, ukiungamanishwa na ule wa baba, ni wenye kudumu milele. Uwezo mkubwa uliopata kuwako humu duniani, tusipohesabu uwezo wake Mungu, ni uwezo alio nao mama kwa ajili ya mema.KN 164.3

    Mama Mkristo daima atakuwa macho kuzijua hatari zinazowazunguka watoto wake. Atauweka moyo wake mwenyewe katika hali safi, na takatifu; atatawala hasira yake na kanuni zinazoyaongoza maisha yake kwa Neno la Mungu naye atafanya kwa uaminifu wajibu wake, akiyashinda majanbu madogo madogo ambayo daima yatamshambulia.KN 164.4

    Akili za watoto ni nyepesi, nao hutofautisha sauti za uvumilivu, na upendo na amri kali ya hasira, ambayo hukausha upendo na nia njema mioyoni mwa watoto. Mama Mkristo wa kweli hatawafukuza watoto wake machoni pake kwa ukali wake na kukosa huruma.KN 164.5

    Akina mama, jueni kwamba mvuto na kielelezo chenu huwa na matokeo kwa tabia na hali ya baadaye ya watoto wenu; na kwa habari ya madaraka yenu, kuzeni nia njema na tabia safi, mkionyesha tu ukweli, wema, na uzuri.KN 165.1

    Wanaume na watoto walio wengi wasiopata cho chote cha kuwavutia nyumbani, ambao daima husalimiwa kwa kushutumiwa na kunung’unikiwa, hutafuta raha na starehe mahali pengine mbali na nyumbani, ulevini au mahali penginepo penye mambo ya anasa yanayokatazwa. Mke ambaye ni mama, akiwa na shughuli nyingi za nyumbani, mara nyingi hajali adhabu ndogo ndogo zifanyazo nyumbani pawe mahali pa kupendeza kwa mumewe na kwa watoto, hata kama asipoyatafakari masumbuko na shida mbele yao. Akiwa katika shughuli ya kutayarisha chakula au nguo, mumewe na wanawe huingia na kutoka kama wageni.KN 165.2

    Kama akina mama wakikubali kuvaa mavazi ovyo nyumbani, wanawafundisha watoto wao kuiga njia hiyo hiyo ya uzembe. Mama walio wengi hudhani kuwa kitu cho chote chatosha kuvaa nyumbani, hata kama ni nguo iliyoraruka vibaya na mbovumbovu. Lakini mara hupotewa na mvuto wao kwa watu wa nyumbani. Watoto huulinganisha mvao wa mama yao na ule wa wengine wenye kuvaa maridadi, na heshima yao kwake hupungua.KN 165.3

    Mke halisi na mama wa watoto atafanya kazi zake kwa makini na moyo wa furaha, bila kufikiri kwamba ni jambo la kumwondolea heshima kufanya kwa mikono yake mwenyewe cho chote kilicho cha lazima kufanywa katika nyumba yenye utaratibu mzuri. 2AH 232-254;KN 165.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents