Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wazazi, Fanyeni Kazi Pamoja kwa Ajili ya Wokovu wa Watoto Wenu

    Pazia lingeweza kurudishwa nyuma na baba na mama waone kama Mungu aonavyo kazi ya siku hiyo, na kuona jinsi jicho la Mungu liilinganishavyo kazi ya mmoja na ile ya mwingine, wangeshangazwa na mafunuo ya mbinguni. Baba angeziona kazi zake dhahiri kidogo, ambapo mama angekuwa na moyo mpya na kupata nguvu kuendesha kazi yake kwa busara. Wakati baba alipokuwa akishughulika na mambo ambayo hayana budi kupotea na kupita, mama amekuwa akishughulika na kukuza akili za moyoni na tabia, akifanya kazi licha ya mambo ya muda mfupi tu, bali hata kwa ajili ya uzima wa milele. 4AH 233;KN 166.3

    Kazi ya baba watoto wake haiwezi kuhamishwa na kupewa mama. Kama mama akifanya kazi yake mwenyewe, anao mzigo wa kutosha kuchukua. Kwa kushirikiana tu kazini ndivyo baba na mama wawezavyo kuitimiza kazi ambayo Mungu amewakabidhi.KN 167.1

    Baba asitoe udhuru kwa kukosa kufanya sehemu yake ya kazi ya kuwafundisha watoto wake kwa ajili ya maisha haya na kwa ajili ya uzima wa milele. Hana budi kushiriki wajibu huu. Wote wawili, baba na mama wana wajibu uwapasao. Yafaa pawepo upendo na staha ambayo huonyeshwa na wazazi wao kwa wao, kama wakipenda kuona tabia hizi kwa watoto wao.KN 167.2

    Baba wa wavulana apaswa afahamiane sana na wanawe, akiwanufaisha kwa maarifa yake mengi zaidi na kuzungumza nao kwa uelekevu na upole ili kuwafungamanisha moyoni mwake. Yampasa aache waone kuwa anawafikiria sana, na ya kuwa furaha yao huikumbuka daima.KN 167.3

    Mwenye jamaa ya watoto wa kiume yampasa kufahamu kuwa, ajapokuwa ana kazi ya namna gani, kamwe asikose kuzijali roho alizopewa kuzitunza. Amewazaa watoto hawa ulimwenguni naye amejitwisha mzigo huu kwa Mungu kufanya kila kitu awezavyo kuwaepusha wasishirikiane na watenda mabaya wala kufanya urafiki nao. Haimpasi kuwaacha watoto wake wa kiume, watundu, kutunzwa tu na mama. Huo ni mzigo sana kwake. Hana budi kupanga mambo kwa faida ya mama na watoto hasa. Pengine itakuwa vigumu sana kwa mama kujitawala na kuyamudu vizuri mafundisho ya watoto wake. Kama ni hivyo, baba angechukua mzigo huo zaidi moyoni mwake. Yampasa akate shauri kujitahidi sana kuwaokoa watoto wake. 5AH 216-221;KN 167.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents