Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wajibu wa Wazazi Katika Kuwafundisha Watoto

    Wafundishe watoto wako kuwa Mungu anadai kwa haki vyote walivyo navyo, na ya kwamba hakuna cho chote kiwezacho kulifuta dai hili; vyote walivyo navyo ni mali waliyodhaminiwa tu, ili kuhakikisha kama watakuwa watiifu. Fedha ni mali itakikanayo; basi, isitapanywe ovyo kwa wale wasioihitaji. Kuna mwenye haja ya vipaji vyako vya ukarimu. Kama u mharibif’u wa mali, punguza gharama za kupita kiasi maishani mara moja. Usipofanya hivi, utafilisika milele. 9CG 134;KN 177.2

    Vijana wa siku hizi hudharau kujiwekea akiba nao huchanganya neno hili na ubahili na choyo. Lakini kujiwekea akiba hupatana na maoni ya akili nyingi na ya ukarimu; hapawezi kuwako ukarimu wa kweli bila ya uwekaji akiba. Mtu awaye yote asidhani kuwa hahitaji kujifunza kuweka akiba kwa njia zilizo bora za kutunza sehemu ndogo ndogo za mali. 1057400KN 177.3

    Basi kila kijana na kila mtoto afundishwe siyo kushinda shida za kuwaziwa tu, bali kuandika hesabu sahihi za mapato na matumizi yake mwenyewe. Ajifunze matumizi halali ya feaha kwa kuitumia. Wakipewa fedha na wazazi wao au wakiipata kwa kufanya kazi wao wenyewe, wavulana na wasichana na wajifunze kuchagua na kununua nguo zao wenyewe, vitabu vyao na mahitaji yao mengine; na kwa kuandika hesabu ya gharama zao, watajifunza kwa njia bora zaidi ya yo yote nyingine, thamani na matumizi ya pesa. 11CS 294;KN 177.4

    Kuna jambo kama lile la kuwapa msaada watoto wetu bila kutumia akili. Wale wanaojilipia gnarama katika vyuo vikuu huthamini majaliwa waliyo nayo zaidi ya wale wanaolipiwa gharama na mtu mwingine, maana hujua inavyowagharamu. Tusibebe mzigo wa watoto wetu kupita kiasi hata kuwafanya wasiweze kujisaidia wenyewe. Wazazi nufanya kosa wanapotoa tu fedha kumpa kijana ye vote mwenye nguvu za kusudi aingie masomoni apate kuwa mhubiri au mganga kabla hajajua kazi ya juhudi iliyo na manufaa. 12AH 387;KN 177.5

    Mazoea ya anasa au mke na mama kukosa kuumia akili huenda ikawa sababu ya upotevu wa mali; lakini mama huyo pengine hudhani kwamba afanya vizuri awezavyo kwa sababu nakufundishwa kutopoteza fedha kwa mahitaji yake au mahitaji ya watoto wake, naye hana ujuzi wala maarifa ya mambo ya nyumbani. Hivyo nyumba moja yaweza kuhitaji msaada maradufu ya ule ambao ungetosha jamaa nyingine kubwa sawa na hiyo. Mungu amependezwa kunionyesha maovu yaletwayo na mazoea mabaya ya kuponda mali, kusudi nipate kuwaonya wazazi kuwafundisha watoto wao kujiwekea akiba. Wafundisheni kuwa fedha inayotumiwa kwa kile wasichohitaji hasa imetumiwa kwa upotevu. 13AH 374, 375;KN 177.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents