Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 28 - Kazi za Familia Wakati wa Likizo na Sikukuu

    NALIONA kuwa likizo zetu zisingetumiwa kama zile walimwengu, walakini zisingekosa kujaliwa, maana hili halitawapendeza watoto wetu. Katika siku hizi zenye uwezekano wa kuwahatarisha watoto wetu kwa mivuto mibaya na kuharibiwa na anasa na starehe za dunia, hebu wazazi watafute kwa bidii kupata kitu kingine badala ya hiyo michezo na starehe zenye hatari zaidi. Wafahamisheni watoto wenu kwamba mnawatakia mema na furaha.KN 179.1

    Kwa kuadhimisha likizo walimwengu na watu wa kanisa wamefundishwa kusadiki kuwa siku hizi za kujikalia kivivu, bila kufanya kazi ni za lazima kwa afya na raha, lakini matokeo yake huonyesha kuwa zimejaa uovu. Tumejaribu sana kuzifanya siku za likizo ziwe zenye kupendeza iwezekanavyo kwa vijana na watoto, huku tukibadili kidogo utaratibu wa mambo. Kusudi letu liwe kuwaepusha na anasa zinazoonekana miongoni mwa wale wasioamini.KN 179.2

    Baada ya siku ya kujipendeza kwa anasa, wapi kuridhika kwa mwenye kupenda anasa? Kama watenda kazi Wakristo, ni nani waliyemsaidia kupata maisha bora zaidi, na sifa zaidi? Wangeweza kuona nini ikiwa wangetazama habari ambazo malaika ameziandika? Siku hiyo haina faida kazini mwa Kristo, kwa sababu hakuna jema lo lote walilotenda. Wanaweza kuwa na siku zingine lakini si hiyo tena ambayo imepishwa kwa mazungumzo yasiyo na maana, ya kijinga, ya wasichana na wavulana, na wavulana na wasichana.KN 179.3

    Kamwe nafasi hizo hazitapatikana tena. Afadhali kama wangefanya kazi ngumu ya juhudi katika likizo hiyo. Maana hawakuitumia vizuri likizo yao nayo imepita milele kuwakabili hukumuni kama siku isiyotumiwa kwa faida.KN 179.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents