Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siku Kuu za Kuzaliwa-wakati wa Kumsifu Mungu

    Katika mfumo wa Kiyahudi kuhusu kuzaliwa kwa watoto sadaka ilitolewa kwa Mungu, kwa agizo lake Mwenyewe. Sasa twaona wazazi wakijisumbua hasa kuwapa zawadi watoto wao katika siku kuu za kuzaliwa kwao. Wanaufanya huu kuwa wakati wa kumtukuza mtoto, kana kwamba mtu ndiye mwenye kustahili sifa. Shetani amepata nafasi katika mambo haya; amezipotosha akili za moyoni na vipaji kwa wanadamu; hivyo mawazo ya watoto yamepotoshwa kujifikiri wenyewe, kana kwamba wao ndio watu wa kusherehekewa hasa.KN 180.5

    Katika sikukuu za kuzaliwa watoto wangefundishwa kwamba wana sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya wema wake katika kuyalinda maisha yao mwaka mwingine. Mafundisho ya thamani yaweza kutolewa kwa njia hii. Kwa ajili ya maisha, afya, chakula, na mavazi na kwa ajili ya matumaini ya uzima wa milele pia, tunawiwa na Mtoaji wa vipaji vyote vya rehema; na Mungu ana haki kupewa shukrani na sadaka zetu za shukrani kwa alivyotukirimia. Sadaka hizi za siku kuu ya kuzaliwa humpendeza Mungu.KN 180.6

    Wafundishe kuyakumbuka mambo ya mwaka uliopita wa maisha yao, wafikiri kama wangependezwa kukutana na habari zake kama zilivyo vitabuni mbinguni. Wasaidie mawazoni wafikiri kama tabia yao, maneno yao, matendo yao, ni yenye kumpendeza Mungu. Je, wameyafanya maisha yao yapate kufanana zaidi na yale ya Yesu, mazuri na yenye kupendeza machoni pa Mungu? Wafundishe kumjua Mungu, njia zake na maagizo yake.KN 181.1

    Nimekwisha kuwaambia watu wa nyumbani mwangu na marafiki zangu, ningependa asiwepo mtu awaye yote anayenipa zawadi ya siku ya kuzaliwa kwangu au zawadi ya sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo (Chrismas), isipokuwa ananiruhusu kuipitisha ipate kuingia katika hazina ya Bwana, ikatumike kuendesha kazi ya utume. 1 AH 472 - 476KN 181.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents