Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kanuni za Mavazi

    Vazi na mshono wake mwilini mwa mtu kwa kawaida huonekana kuwa kielelezo cha hali ya mwanamume au mwanamke.KN 204.4

    Twafahamu tabia ya mtu kwa namna ya mavazi anayovaa. Mwanamke mwenye adabu, mcha Mungu atavaa kwa adabu. Akili nzuri, moyo wa uadilifu, utadhihirishwa katika kuchagua mavazi yanayofaa, yasio na mapambo mengi. Mtu ambaye si mwenye kiburi katika mavazi yake na hali yake huonyesha kuwa anafahamu kwamba mwanamke wa kweli huainishwa na uadilifu. Kutojipamba kwa mavazi ni jambo la kupendeza sana, ambalo kwa uzun laweza kulinganishwa na maua ya kondeni.KN 204.5

    Nawasihi watu wetu kuenenda kwa uangalifu na kwa tahadhari mbele za Mungu. Igeni namna ya mavazi kadiri inavyopatana na kanuni za afya. Hebu dada zetu wavae pasipo urembo, kama wengi wafanyavyo, wakiwa na mavazi mazuri, ya vitambaa vidumuvyo, vya kufaa siku hizi; tena mavazi yasiwe jambo kubwa mawazoni. Yawapasa wajivike nguo za adabu, kusetiri aibu ya uchi na kuwa na kiasi. Wapeni walimwengu kielelezo cha nguvu cha kujipamba kwa neema ya Mungu.KN 204.6

    Kama walimwengu wakianzisha namna ya mavazi ya adabu ya kufaa, na yenye kukidhi afya, yanayopatana na Biblia, haitadhuru uhusiano wetu na Mungu ama na walimwengu kuiga mtindo wa namna hiyo. Wakristo wangemwiga Kristo na kufanya uvaaji wao kupatana na Neno la Mungu. Wawe na kiasi. Kwa unyenyevu wangefuata unyofu, wasijaii sifa, wala lawama; yafaa washikilie kutenda mema kwa sababu ya uzuri wa wema huo.KN 204.7

    Usijisumbue wakati wote kwa kujaribu kuiga namna zote za mavazi zisizo na maana. Vaa nguo safi na nzuri, lakini usijionyeshe ama kwa kuvaa maridadi kiasi ama kwa kuvaa vibaya, kwa uzembe. Tenda kana kwamba unajua kuwa jicho la mbinguni linakutazama, na ya kuwa unaishi chini ya kibali cha Mungu ama kinyume na mapenzi yake. 2CG 413-415;KN 205.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents