Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mafundisho ya Biblia

    Kristo aliona upendo wa mavazi, naye alionya, naam, akaamuru wafuasi wake wasiyafikiri sana hayo. “Na mavazi ya nini kuyasumbukia? Fikiri maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.” Kiburi na upotevu wa mali katika mavazi ni dhambi ambayo mwanamke hupenda hasa; hivyo maagizo haya humhusu yeye hasa. Dhahabu au lulu au nguo za thamani kubwa ni vyenye thamani ndogo sana vikilinganishwa na upole na uzuri wa Kristo!KN 205.2

    Nalielekezwa kwenye Maandiko naya yafuatayo. Malaika akasema, “Yapasa kuwafundisha watu wa Mungu. “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitin, pamoja na adabu nzuri, la moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu” (1 Timotheo 2:9, 10).KN 205.3

    “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upde na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana nivyo ndivyo walivyo jipamba wanawake watakatifu wa zamani” (1 Petro 3:3-5).KN 205.4

    Wengi huyadharau maagizo hayo na kuyahesabu kuwa ya zaman sana hata haina maana kuyajali; lakini Mwenye kuyatoa kwa wanafunzi wake alijua hatari zitokanazo na kupenda mavazi siku zetu, akatupelekea onyo kubwa. Je, tutalitii onyo hilo na kuwa wenye hekima?KN 205.5

    Wale wanaotafuta kwa kweli kumfuata Kristo watajihadhari sana ra mavazi wavaayo; watajitahidi kutimiza masharti ya agizo hilo lililotolewa wazi na Bwana (1 Petro 3:3-5). 3CG 415, 416;KN 205.6

    Kiasi katika kuvaa ni sehemu ya wajibu wetu wa Kikristo. Kuvaa bila kujipamba, kuepukana na kujipamba kwa johari na mapambo ya kila namna, ni jambo linalopatana na imani yetu.KN 205.7

    Wengi huhitaji mafundisho jinsi iwapasavyo kuonekana katika mikutano ya ibada siku ya Sabato. Haiwapasi kuingia mahali Mungu alipo wakivaa mavazi ya kawaida yaliyovaliwa siku za kazi katika juma hilo. Yafaa wote kuwa na mavazi maalumu ya Sabato yavaliwayo wakienda kuhudhuria ibada nyumbani mwa Mungu. Huku tukiwa hatupaswi kuiga mitindo ya kilimwengu, tusikose kujali hali yetu ya nje. Yatupasa tuwe maridadi, ingawa hatujipambi. Yafaa watoto wa Mungu wawe safi ndani na nje. 56T 355;KN 206.1

    Akili za moyoni huelekeza huko. Hiyo ndiyo sababu Wakristo huyaona maisha ya dini kuwa magumu sana na maisha ya kidunia kuwa rahisi sana. Akili zimezoezwa kutoa nguvu yake upande huo. Katika maisha ya kidini pamekuwako ukubali wa maneno ya kweli ya Biblia, lakini siyo kutendeka halisi kwa maneno hayo maishani.KN 206.2

    Kukuza mafikara ya dini na moyo wa kumwabudu Mungu haifanywi kuwa sehemu ya mafundisho. Hayo yangeongoza na kuutawala mwili nzima. Mazoea ya kutenda mema hayapo. Kuna utendaji wa ghafla kwa mivuto mizuri, lakini kufikiri siku zote kwa urahisi juu ya mambo matakatifu si kanuni inayotawala akilini.KN 206.3

    Akili za moyoni hazina budi kufundishwa na kuongozwa kupenda usafi. Upendo wa mambo ya kiroho ungetiwa nguvu; naam, hauna budi kutiwa nguvu, kama wakipenda kukua katika neema na kuujua ukweli. Tamaa ya wema na utakatifu wa kweli ni nzuri kadiri llivyo; lakini ukikoma hapo, haitakufaa cho chote. Makusudi mema hufaa, lakini hayatakuwa na maana kama vasipotimizwa kwa uthabiti. Wengi watapotea wakiwa wanatumaini na kutamani kuwa Wakristo; lakini hawajitahidi kwa moyo, hivyo watapimwa kwa mizani na kuonekana kuwa wamepungua. Nia haina budi kutumiwa kwa upande mzuri. Nitakuwa Mkristo kwa moyo wangu wote. Nitajua urefu na mapana, kimo na kina cha upendo kamili. Hebu yasikilize maneno ya Yesu: “Heri wenye njaana kiu ya haki; maana hao watashibisnwa.” Mathayo 5:6. Majaliwa makubwa hutolewa na Kristo kuiridhisha roho ya mtu mwenye njaa na kiu ya haki. 3CG 415, 416;KN 206.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents