Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuchuchumia Mambo ya Kiroho Yaliyo Bora Zaid

    Kiini safi cha upendo kitaipanua roho ya mtu ili kutoanafasi kwa mambo bora zaidi, kwa ongezeko la maarifa ya mambo yi kiroho, kusudi isiridhike na hali pungufu. Wengi wanaodai ni Wakristo hawajui nguvu za kiroho ambazo wangaliweza kuzipata kama wangekuwa wenye nia, wenye bidii, na kujitahidi kupata ujuzi wa mambo matakatifu kama wafanyavyo kupata mambo hafifu valiyo ya kitambo tu katika maisha haya. Jamii ya watu wanaojidai kuwa ni Wakristo wameridhika kudumaa kiroho. Hawana nia kulifanya kusudi lao kuwa kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake; kwa kuwa utauwa ni siri iliyofichwa kwao, hawawezi kuifahamu. Hawamjui Kristo wa Hakika.KN 206.5

    Wanaume na wanawake waridhikao na hali yao ya kudumaa na kuwa vilema katika mambo ya kiroho hebu wapelekwe mbinguni kwa ghafla waone kwa macho hali timilifu, bora na takatifu iliyoko kule daima kila nafsi imejawa na upendo; kila uso uking’aa kwa furaha; muziki wakupendeza sana kwa sauti tamu zinazolingana vizuri za kumtukuza Mungu na Mwana Kondoo; na nuru lsiyokoma ikiwazukia watakatifu kutoka usoni mwake Aketiye juu ya kiti cha enzi, na kutoka kwa Mwana Kondoo; basi, nawatambue kuwa kuna furaha kubwa zaidi bado ya kufaidi, maana kadiri wazidivyo kupokea furaha ya Mungu, ndivyo nafasi yao inavyoongezeka kupanda juu kwenye ile furaha ya milele, na kwa njia hiyo kuendelea kupokea manufaa mapya na makubwa zaidi kutoka katika machimbuko yasiyokoma ya utukufu na mbaraka usioelezeka -Nauliza, watu kama hao waweza kuwa miongoni mwa mkusanyiko wa mbinguni, kushiriki nyimbo zao, na kufaidi utakatifu, na utukufu bora utokao kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo? Ah, la! Muda wao wa majaribio kama wanafaa au hawafai ulizidishwa miaka mingi ili wapate kujifunza lugha ya mbinguni, kusudi wapate kuwa “washiriki wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharioifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” ( 2 Petro 1:4). Lakini walikuwa na shughuli za miili yao. Hawakuweza kumtumikia Mungu kwa moyo wote na kuhfanya hilo kuwa shughuli yao. Shugruli za dunia hapana budi zilifika kwanza na kutwaa uwezo wao ulio bora na wazo la muda mfupi tu hutolewa kwa Mungu. Watu kama hao watabadilishwa baada ya kukatwa shauri la mwisho: “Mtakatifu na azidi kutakaswa,” “mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu?” Wakati kama huo unakuja.KN 207.1

    Wale ambao wamezizoeza akili zao kuyafurahia mambo ya kiroho ndio watakaoweza kuhamishwa wala wasiangamizwe na usafi la utukufu bora sana wa mbinguni. Pengine unaweza kuwa na maarifa bora ya kazi ya ufundi, ama unaweza kuwa na ujuzi wa elimuya ‘sayansi’, labda unaweza kushinda kwa ubora katika uimbaji na katika mwandiko, ama tabia yako ikawapendeza marafiki zako, lakini mambo hayo yanahusiana na matayarisho ya kwenda mbinguni? Yanahusiana na kukutayarisha kusimama mbele ya baraza la hukumu ya Mungu? 43T 366;KN 207.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents