Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 35 - Ombi kwa Vijana

    VIJANA rafiki wependwa, kila mnachopanda mtakivuna pia. Sasa ni wakati wenu wa kupanda. Mavuno yatakuwaje? Mwapanda nini? Kila neno msemalo, kila tendo mtendalo, ni mbegu ambayo itazaa matunda mema au mabaya, nayo italeta furaha au huzuni kwa mpandaji. Kama ilivyo mbegu iliyopandwa, ndivyo yatakavyokuwa mavuno. Mungu amewapa nuru kubwa na mibaraka mingi. Baada ya nuru hiyo kutolewa, baada ya hatari kuonyeshwa dhahiri mbele yenu, mambo yanabaki juu yenu. Namna mnavyofanya na nuru ambayo mnapewa na Mungu italetsa furaha ama huzuni. Ninyi wenyewe mnajitayarishia mwisho wenu wenyewe.KN 212.1

    Nyote mna mvuto wa mema ama wa mabaya katika akili zetu za moyoni na kwenye tabia za wengine. Na mvuto mnaoutoa huandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbinguni. Malaika anafuatana nanyi kila mwendako na kuandika habari za maneno na matendo yenu. Mnapoamka asubuhi, mwauona udhaifu wenu na hitaji lenu la nguvu kutoka kwa Mungu? Je, kwa moyo mnyenyekevu mwayafanya mahitaji yenu kujulikana kwa Baba yenu aliye mbinguni? Kama mwaranva hivyo, malaika hutazama sala zenu, na ikiwa sala hizo hazijatoka katika midomo ya kusingizia, wakati mkiwa katika hatari ya kufanya mabaya bila kujua na kutoa mvuto utakaowaongoza wengine kufanya mabaya, malaika akulindaye atakuwa karibu nawe kukusaidia kutenda mema, akikuchagulia maneno, na kuongoza matendo yako.KN 212.2

    Kama hujioni hatarini, na ikiwa huombi kwa Mungu msaada na nguvu kuyapinga majaribu, bila shaka utapotea; kutojali wajibu wako kutaonyeshwa katika kitabu cha Mungu mbinguni, nawe utaonekana umepungua siku ile ya kupimwa.KN 212.3

    Wako wengine pande zote kukuzunguka ambao wameongozwa kwa jinsi lpasavyo watu wenye dini na wengine ambao wameendekezwa, wakapendelewa, wakasifiwa isivyostahili, na kutukuzwa mpaka wameharibika hata hawafai hata kidogo maishani. Nasema juu ya watu niwajuao hasa tabia zao zimepotoshwa sana na anasa, sifa za bure, na uvivu hata hawana faida katika maisha haya. Na ikiwa hawafai kitu kwa maisha haya, twaweza kutumaini nini kwa yale maisha ambayo wote ni safi na watakatifu, na ambayo wote watakuwa wenye tabia zinazopatana? Nimewaombea watu hao; nimezungumza nao mimi mwenyewe. Naliweza kuona mvuto ambao wangeweza kuwatolea watu wengine katika kuwapotosha, upendo wa mavazi, kutojali mambo yao ya milele. Tumaini la pekee kwa watu wa aina hiyo ni wao wenyewe kujihadhari na njia zao, kunyenyekea mioyoni mwao na kuachana na kiburi cha bure mbele za Mungu, kuziungama dhambi zao, na kuongoka. 13T 363, 364;KN 212.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents