Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ubaya wa Uvivu

    Nimeonyeshwa kuwa dhambi nyingi zimetokana na uvivu. Mikono na bongo hodari kwa kazi hazina nafasi kusikiliza kila jaribu ambalo adui huwaletea, lakini mikono na bongo zenye uvivu ziko tayari kabisa kutawaliwa na Shetani. Akili, isiposhughulishwa vizuri, hufikiri mambo mabaya yasiyofaa. Yawapasa wazazi wawafundishe watoto wao kuwa uvivu ni dhambi. 161T 395;KN 220.1

    Hakuna jambo linaloelekea sana kutia maovuni zaidi ya kuwaondolea watoto mizigo yote, kuwaacha kuishi kivivu, bila shabaha yo yote, kutofanya lolote, ama kufanya kama wanavyopenda. Akili za watoto zina kazi, na kama zisiposhughulishwa kwa lile lililo jema na lenye manufaa, bila shaka zitageukia baya. Huku likiwa jambo zuri na la muhimu kwao kuwa na michezo wangefundishwa kufanya kazi, kuwa na saa za kawaida kwa kazi ya juhudi na pia kwa kusoma na kujifunza. Ona kwamba wanayo kazi inayowafaa kwa maisha yao na ya kwamba wanapatiwa vitabu vya kufaa vyenye kuwapendeza. 17AH 284;KN 220.2

    Mara kwa mara watoto huanza kipande cha kazi kwa bidii; lakini, wakitatizwa au kusumbuliwa nayo, hutamani kubadili na kuanza kufanya kitu kingine kipya. Hivyo huenda wakaanza kufanya mambo mengi, walcikutana na jambo la kuwakatisha tamaa, na kuyaacha; kwa hiyo, huacha hili na kuanza kufanya lingine, bila kukamilisha kitu cho chote. Wazazi wasikubali moyo wa kupenda kubadilibadili ukawatawala watoto wao. Haifai washughulikie mambo mengine hata kukosa nafasi kutawala kwa uvumilivu na kukuza akili za watoto. Maneno machache ya kutia moyo au msaada kidogo kwa wakati wa kufaa, huweza kuwaepusha na taabu na tabia ya kukata tamaa; na kuridhika kutakakotokana na kazi waliyoifanya na kuitimiza vizuri kutawatia nguvu kufanya bidii kwa kazi kubwa zaida. 183T 147, 148;KN 220.3

    Watoto ambao wameendekezwa na kungojewa, siku zote huitazamia; na kama matumaini yao yasipotimizwa hukatishwa tamaa na kufa moyo. Tabia ya namna hiyo hiyo itaonekana katika maisha yao yote; watakuwa dhaifu, wakiwategemea wengine kwa msaada, wakiwatazamia wengine kuwapendelea na kujitoa kwao. Na kama wakipingwa, hata baada ya kwisha kuwa watu wazima wa kiume na wa kike, wanafikiri kwamba wanatendwa vibaya; na kuharakisha kuingia katika anasa za ulimwengu, na kushindwa kujitegemea; mara nyingi hunung’unika na kuhangaika kwa sababu mambo yote yanawaendea vibaya. 191T 392, 393;KN 220.4

    Mwanamke hujifanyia vibaya yeye mwenyewe na pia huwafanyia kosa baya watu wa nyumba yake, akifanya kazi yake na pia akileta kuni na maji, na hata kuchukua shoka ili kuchanja kuni, uku mumewe na wanawe wakakaa mekoni wakistarehe. Kamwe Mungu hakukusudia kwamba wake na mama wawe watumwa wa jamaa zao. Mama wengi husumbuliwa kupita kiasi huku watoto wake wakiwa hawafundishwi kushiriki mizigo ya nyumba. Kama matokeo yake, huzeeka na kufa mapema kabla ya uzee, na kuwaacha watoto wake wakati wake wakati mama anapotakikana sana kuiongoza miguu yao isiyojua kitu. Ni nani astahiliye kulaumiwa?KN 220.5

    Yafaa wanaume kufanya yote wawezayo kuwaepusha wake na taabu na kuwafanya wastarehe. Kamwe uvivu usipendelewe wala kuruhusiwa kwa watoto, maana upesi huwa mazoea. 205T 180, 181;KN 221.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents