Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wazazi, Waongozeni Watoto Wenu kwa Kristo

    Pengine watoto watataka kutenda mema, huenda wakakusudia mioyoni mwao kuwa watiifu na wema kwa wazazi au walezi wao; lakini huhitaji msaada na maneno ya kuwatia moyo. Wanaweza kuwa na makusudi mema; lakini kama kanuni zinayoyaongoza maisha yao zisipotiwa nguvu kwa dini na maisha yao kuongozwa na neema ya Mungu itiayo nguvu, watashindwa kufaulu.KN 221.2

    Yawapasa wazazi kuzidisha maradufu jitihadi zao kwa ajili ya wokovu wa watoto wao. Wangewafundisha kwa uaminifu, wasiwaache kuokota mafundisho yao huko na huko kama wawezavyo. Haifai watoto wadogo kuachwa kujifunza mema na mabaya ovyo bila kutumia busara, kwa kudhani kwamba baadaye mema yatakuwa na nguvu na mabaya yatakosa nguvu. Maovu yatazidi kuongezeka upesi kuliko mema.KN 221.3

    Wazazi, mngeanza kuzitawala akila za watoto wenu wakati wangali wadogo sana, hadi mwisho ili wapate kuwa Wakristo. Jitihada zenu zote ziwe kwa ajili ya wokovu wao. Fanyeni kama kwamba wamekabidhiwa kwenu kufanywa wafae kama vito vya thamani kung’aa katika ufalme wa Mungu. Jihadharini msiwatie usingizi wakalala wakiwa katika hatari ya kuangamia kwa kukosea mkidhani kuwa si wenye umri wa kutosha kuwa na hatia, wala wakubwa wa kutosha kutubia dhambi zao na kumkiri Kristo.KN 221.4

    Yafaa wazazi kueleza na kuurahisisha mpango wa wokovu kwa watoto wao kusudi akili zao changa zipate kuufahamu. Watoto wa miaka nane, kumi, au kumi na miwili ni wakubwa wakutosha kuzungumuziwa somo la dini la pekee. Msiwafundishe watoto wenu na kuwaelekeza kwenye wakati fulani ujao ambapo watakuwa wakubwa na kutosha; wadogo sana huweza kuona vizuri hali yao kama wakosaji na njia ya wokovu upatikanao kwa Kristo. Wachungaji mara nyingi hawajali hata kiaogo wokovu wa watoto wao; hawafanyi wajibu wao. Nafasi nzuri kuyavuta mawazo ya watoto mara nyingi hupitwa bila kutumiwa vizuri kwa manufaa. 2177 396 - 400;KN 221.5

    Akina baba na mama, mwafahamu ukubwa wa wajibu wenu? Mwajua inavyowapasa kuwalinda watoto wenu na mazoea ya uzembe yanayoharibu tabia? Msiwaruhusu kutoka nje saa za jioni kama msipojua mahali walipo na kile wanachofanya. Wafundisheni kanuni za usafi wa tabia ya adili. Ikiwa hamkujali kuwafundisha amri juu ya amri, kanuni, nuku kidogo na huku kidogo, anzeni mara moja kufanya wajibu wenu. Twaeni madaraka yenu na kufanya kazi kwa ajili ya muda kitambo na kwa ajili ya milele pia. Msikubali siku nyingine ikapita kabla ya kuungama kosa la kutowajali watoto wenu. Waambieni kuwa mnananuia sasa kutenda kazi mliyopewa na Mungu. Waombeni kushikamana nanyi katika kuongoka nuko. Fanyeni bidii kukomboa mambo ya wakati uliopita. Msikae tena katika hali ya kanisa la Laokidia. Kwa jina la Bwana nawasihi watu wa kila nyumba kujidhihirisha kama ilivyo hasa. Tengeneza kanisa nyumbani mwako mwenyewe. 227T 66, 67;KN 222.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents