Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kamwe Usiwarudi Watoto Ukiwa Umekasirika

    Kama watoto wako ni wahalifu, wangeadhibiwa. Kabla ya kuwaadhibu, jitenge, na kumwomba Mungu kuilainisha na kuituliza mioyo ya watoto wako na kukupa hekima katika kushughulika nao. Kamwe sijaona njia hii kushindwa kufaulu. Huwezi kumfahamisha mtoto mambo ya kiroho wakati moyo (moyo wa mzazi) umejawa na hasira.KN 223.2

    Ungewatia adabu watoto wako kwa upendo. Usiwaache kufanya wapendavyo mpaka ukasirike, ndipo kuwarudi. Kuwarudi kwa njia hiyo husaidia tu mabaya, badala ya kuyaponya.KN 223.3

    Kuonyesha ukali kwa mtoto mkosaji ni kuzidisha ubaya. Huamsha hasira mbaya ya mtoto na kumwongoza kuona kuwa humjali. Hufikiri kimoyomoyo kuwa usingemtenda hivyo kama ungemjali.KN 223.4

    Je, unadhani kwamba Mungu haangalii njia ambayo kwayo watoto hao hutiwa adabu? Ajua, tena ajua kile ambacho kingekuwa matokeo bora ikiwa kazi ya kuwarudi ingefanywa kwa njia ya kuwapata badala ya kuwafukuza. 24 CG 244, 245;KN 223.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents