Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ukubwa wa Kuwatendea Watoto Haki Kabisa

    Yafaa wazazi wawe vielelezo vya uaminifu, maana hili ndilo fundisho la kila siku la kukuzwa moyoni mwa mtoto. Kanuni imara ingetawala wazazi katika mambo yote ya maisha, hasa katika mafundisho na malezi ya watoto wao. “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.”KN 224.1

    Mama asiye na busara, asiyefuata maongozi ya Mungu, aweza kuwafimdisha watoto wake kuwa wadanganyifu na wanaiiki Dalili za tabia ya namna hiyo zikihifadhiwa zaweza kuendelea bila kubadilika hata kusema uongo kuwe jambo la kawaida kama vile kupumua. Kujisingizia kutakuwa badala ya unyofu na hakika.KN 224.2

    Wazazi, kamwe msitoe maneno ya ujanja; kamwe msiseme uongo kwa mafundisho wala kwa kielelezo. Kama wataka mtoto wako awe mwaminifu, uwe mwaminifu wewe mwenyewe. Uwe mnyofu asiyekwenda upande. Hata ujanja kidogo usikubaliwe. Kwa sababu mama anazoea kutoa maneno ya ujanja na kuwa muongo, mtoto hukifuata kielelezo cha mama.KN 224.3

    Basi, ni muhimu kwamba uaminifu utumiwe katika mambo yote ya maisha ya mama, na ni jambo la maana katika malezi ya watoto kuwafundisha vijana wa kike na wa kiume pia wasitoe maneno ya ujanja kudanganya hata kwa neno lililo dogo kabisa. 25CG 151, 152;KN 224.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents