Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Fundisha Heshima na Adabu

    Mungu ameamuru hasa heshima nzuri kwa wazee. Asema, “Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu, kama kikionekana katika njia ya haki” mithali 16:31. Huonyesha vita vilivyokwisha kupiganwa na ushindi uliopatikana; mizigo iliyobebwa, na majaribu yaliyopingwa. Huonyesha miguu iliyochoka ikikaribia pumziko lao, na juu ya mahali ambapo si muda mrefu pataachwa tupu. Wasaidie watoto kufikiri hivyo, nao watayalainisha mapito ya wazee kwa adabu na heshima zao, na watajiletea neema na uzun katika maisha yao ya ujana kadiri wanavyoitii amri huu, “Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee.” Mambo ya Walawi 19::32. 37Ed. 244;KN 228.1

    Pia adabu, ni mojawapo ya karama za Roho, nayo ingekuzwa na wote. Ina nguvu ya kulainisha tabia ambazo pasipo hiyo zingeendelea kuwa nguvu na zisizo za heshima. Wale wanaodai kuwa ni wafuasi wa Kristo, na huku wakiwa watu wasio na adabu, wakali, na wasio na heshima, hawajajifunza bado juu ya Yesu. Pengine unyofu wao hauwezi kuonewa mashaka, wala uaminifu wao kutosadikiwa sana; lakini unyofu na uaminifu hautaridhisha kwa sababu hauna utu wema na adabu. 38PK 237KN 228.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents