Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Msaada wa Tabia ya Uadilifu katika Vyuo Vyetu

    Yafaa baba na mama kushirikiana na mwalimu kazini kwa bidii kwa ajili ya uongofu wa watoto wao. Hebu wajitahidi kudumisha moyo wa kupendezwa na mambo ya kiroho na matakatifii nyumbani na kuwalea watoto wao katika malezi na maonyo ya Bwana. Hivyo ndivyo wawezavyo kuifanya saa ya mafimdisho kuwa ya kupendeza na yenye faida, na matumaini yao yataongezeka kwa njia hii ya kuutafuta wokovu wa watoto wao. 126T.199;KN 231.5

    Baadhi ya wanafunzi hurejea nyumbani wakiwa na manung’uniko, na wazazi na washiriki wa kanisa huyasikiliza maneno yao yaliyotiwa chumvi, yasiyo ya haki. Ingekuwa bora kama wangefikin kuwa hadithi ina pande mbili; lakini badala ya kufanya hivyo, hukubali rioti hizo zilizopotoka kujenga kizuizi baina yao na chuo hicho kikuu. Ndipo huanza kuonyesha hofu, mashaka, na shuku juu ya njia inayotumiwa kukiendesha chuo hicho. Mvuto wa namna hiyo huleta madhara makubwa. Maneno ya kutoridhika huenea kama ugonjwa unaoambukiza, na ushawishi ufanywao mawazoni ni shida kuuondoa kabisa. Uvumi huzidi kila mara mpaka kuwa mkubwa mno, ambapo uchunguzi ungeonyesha ukweli kwamba walimu hawakuwa na kosa wala walimu wakuu wa chuo hicho. Walikuwa wakifanya tu wajibu wao katika kuzitilia nguvu amri za shule, ambazo hazina budi kutimizwa, ama sivyo shule itachafuliwa.KN 232.1

    Ikiwa wazazi wangejiweka mahali pa walimu na kuona jinsi inavyolazimu kuwa vigumu kuongoza na Kutawala shule ya wanafunzi mamia wa kila darasa na wa aina mbalimbali, huenda wakayaona mambo namna nyingine. Wangefikiri kuwa watoto wengine kamwe hawakupata malezi mema nyumbani. Kama watoto hao ambao wametupwa ovyo na wazazi wasio waaminifu wasipofanyiwa kitendo, kamwe hawatakubaliwa na Yesu; isipokuwa uwezo fulani wa kuwatawala unaletwa kuwasaidia, hawatakuwa na maana katika maisha haya wala hawatashiriki maisha ya wakati ujao. 134T.628,629;KN 232.2

    Baba na mama wengi hukosa kwa kulegeza bidii ya mwalimu mwaminifu. Vijana na watoto, kwa uwezo wa kufahamu usio kamili na maamuzi yao machanga hawawezi siku zote kufahamu mipango na njia zote za mwalimu. Lakini, wanapoleta nyumbani ripoti za mambo yasemwayo na kufanywa katika shule, hayo huzungumzwa na wazazi katika jamii ya watu wa nyumbani, na matendo ya mwalimu hulaumiwa bila kizuizi. Hapo watoto hujifunza mafundisho ambayo si vyepesi kujifunzwa. Wakati wo wote wanapopaswa kujizuia wasivyozoea, au kutakiwa kujifunza mambo magumu, huwalalamikia wazazi wao wasio na busara ili wawahurumie na kuwaendekeza. Hivi ndivyo moyo wa wasiwasi na kutokuridhika unavyotiwa nguvu, na shule nzima huumia kwa sababu ya mvuto huo ambao huichafua na mzigo wa mwalimu huzidi kuwa mzito. Lakini, hasara iliyo kubwa zaidi ni kwa watoto wenyewe wenye kufundishwa hivi na wazazi wao. Makosa ya tabia ambayo malezi mazuri yangeweza kuyasahihisha, huachwa kupata nguvu kadiri miaka iendavyo, kuharibu na pengine kuangamiza kabisa manufaa ya yule aliyo nayo. 14FE.64,65;KN 232.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents