Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Biblia Katika Elimu ya Kikristo

    Kama njia ya kuelimisha, Biblia ni yenye matokeo zaidi ya kitabu kinginecho, au vitabu vyote vingine vikiunganishwa pamoja. Ubora wa maneno yake makubwa, na mepesi kueleweka, uzuri wa maneno yake yanayoleta mifano akilini, hutia nguvu na kukuza akili kuliko cnochote kingine. Hakuna mafundisho mengine yawezayo kutoa elimu kama bidii ya kuyafahamu maneno ya kweli ya mafunuo hayo. Akili ambazo zimeunganishwa na nia ya Mungu jinsi hiyo zitazidi tu kupata nguvu.KN 235.3

    Pia uwezo wa Biblia una nguvu zaidi katika maendeleo ya hali ya kiroho. Binadamu, ambaye ameumbwa kusudi ashirikiane na Mungu, aweza tu kupata uzima na maendeleo yake halisi, kwa ushirika wa namna hiyo. Akiwa ameumbwa kwa namna inayomwezesha kupata fursaha yake ilio bora sana kwa Mungu, kile ambacho chaweza kutuliza kiu cha moyo hawezi kukipata kwa njia nyingine iwayo yote. Yeye ambaye kwa unyofu na uelekevu wa moyo hujifunza Neno la Mungu, akitaka kufahamu ukweli wake, atamfahamu Muumbaji wake; na isipokuwa kwa hiari ya mtu mwenyewe, hakuna kikomo cha uwezekano wa maendeleo yake. 26ED.124,125 ;KN 235.4

    Hebu mafungu ya Maandiko Matakatifu yenye maana inayohusiana zaidi na mafundisho yanayotolewa yakaririwe hata yaweze kukumbukwa, si kama kazi ngumu, bali kama kitu cha faida. Ingawa mara ya kwanza huenda uwezo wa kukimbuka ukawa na upungufu, lakini, utapata nguvu kwa kuzoezwa, ili baada ya muda upendezwe kuyaweka moyoni maneno ya kweli. Nayo mazoea haya yatasaidia sana kukua kiroho. 27CT.137,138 ;KN 235.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents