Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ukubwa wa Mafundisho ya Kazi za Maisha Yenye Manufaa

    Siku hizi, kama ilivyokuwa katika siku za Waisraeli, kila kijana angefundishwa kazi za maisha yenye manufaa. Kila mmoja angejipatia ujuzi wa kazi fulani ya mikono ambayo kwayo, kama ikilazimu, aweza kujipatia maisha yake. Hili ni jambo la muhimu, licha ya kuwa kinga ya mabadiliko ya hali ya mambo ya maisha, bali hata katika uhusiano wake na maendeleo ya mwili, akili na tabia ya moyoni.KN 237.1

    Yafaa ufundi wa kazi mbalimbali ufundishwe shuleni mwetu. Kazi ya kuandika hesabu za fedha, useremala, na mambo yote yapasayo ukulima yafaa yawe miongoni mwa mafundisho ya ufundi wa kazi za mikono. Matayarisho yangefanywa kwa ajili ya kufundisha uhunzi, kupaka rangi, ushonaji wa viatu na upishi, uokaji, udobi; ufundi wa kukarabati vitu vikuukuu, kuandika kwa ‘komputa’, na kuchapisha vitabu. Kila uwezo tulio nao hauna budi kutumiwa katika mafunzo haya ya kazi za maisha yenye manufaa.KN 237.2

    Ziko kazi nyingi kwa ajili ya wanafunzi wasichana ambazo yafaa zifundishwe ili waweze kupata elimu ya maana sana na yenye manufaa mengi. Yawapasa wafundishwe kushona nguo na kulima bustani. Yafaa wapande maua na matunda. Hivyo, huku wakifundishwa kazi za manufaa, watakuwa na mazoezi ya mwili nje ambayo hutia afya. 31CT.307-312;KN 237.3

    Mvuto wa akili mwilini, na ule wa mwili akilini, ungekazwa. Nguvu za upesi ajabu za ubongoni, zikikuzwa kwa utendaji wa akili, hutia nguvu mwili mzima, na kwa njia hii msaada wa thamani sana katika kushindana na ugonjwa hupatikana. Pana ukweli juu ya habari za mwili wa mtu-ukweli ambao twahitaji kuufikiri katika Andiko hili, “Moyo uliochangangamka ni dawa nzuri. 32ED.197 ;KN 237.4

    Ili watoto na vijana wawe na afya, furaha, wepesi, na misuli pamoja na akili zilizoadilishwa, yawapasa wawe nje saa nyingi, na kufanya kazi zinazosimamiwa vizuri pamoja na michezo. Watoto ambao hushindishwa shuleni na kujifunza vitabuni saa zote, hawawezi kuwa na miili yenye afya njema. Mazoezi ya akili katika kujifunza, bila kufanya mazoezi ya viungo vya mwili yanayolingana nayo, huleta damu ubongoni, na mwendo wa damu mwilini hauwezi kuwa sawa. Ubongo huwa na damu nyingi mno, na viungo vingine vya mwili kuwa na damu kidogo sana. Yapasa pawepo amri zinazotawala mafundisho ya watoto na vijana, wajifunze kwa saa fulani tu, kisha sehemu ya wakati wao unaobaki itumiwe katika kazi za juhudi. Tena, kama mazoea yao ya kula, kuvaa, na kulala yanaafikiana na kawaida za afya, wanaweza kupata mafundisho bila kukosa afya ya mwili, na akili. 33CT.83 ;KN 237.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents