Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wajibu wa Mwanafunzi Kusaidia Shule Yake

    Wale wanafunzi wanaodai kumpenda Mungu na kulitii neno la kweli yafaa wajitawale na kuwa na nguvu za kanuni ya dini ambayo itawawezesha kudumu imara katikati ya majaribu na kusimama kumtetea Yesu katika chuo, katika bweni zao, ama po pote walipo. Dini si kitu cha kuvaliwa tu kama joho nyumbani mwa Mungu, bali kanuni za dini hazina budi kuifanyiza tabia ya maisha yote.KN 240.2

    Wale wanaokunywa katika chemchemi ya uzima hawataonyesha tamaa ya mageuzi na anasa, kama walimwengu. Katika mwenendo na tabia yao pataonekana na amani na furaha ambayo wameipata kwa Yesu kwa kuyaweka kila siku mashaka na mizigo yao miguuni pake. Wataonyesna kwamba pana kuridhika na furaha pia katika njia ya utii na kazi. Watu kama hao watatoa mvuto kwa wanafunzi wenzao ambao utadhihirika katika shule nzima.KN 240.3

    Wale walio miongoni mwa jeshi hilo aminifii watawaburudisha na kuwatia nguvu walimu na walimu wakuu katika jitihadi zao kwa kuzuia udanganyifu wa kila aina, fitina, ama kukataa kuzitii amri na kawaida za shule. Mvuto wao utaokoa, na matendo yao hayatapotea katika siku ile kuu ya Mungu, bali yatawafuata kwenye ulimwengu wa wakati ujao; na mvuto wa maisha yao hapa utadnihirika siku zote, milele.KN 240.4

    Kijana mmoja aliye mwaminifu, mwenye bidii kutenda mema shuleni ni hazina kubwa mno. Malaika wa mbinguni humtazama kwa upendo. Mwokozi wake wa ajabu humpenda, na katika Daftari ya Mbinguni pataandikwa kila tendo la haki, kila jaribu lililopingwa, kila dhambi iliyoshindwa. Hivyo ndivyo atakavyoweka msingi mwema kwa ajili ya wakati ujao, kusudi apate kuushikilia uzima wa milele.KN 241.1

    Hifadhi na ufulizo wa shule ambazo Mungu ameziazimia ziwe njia ya kuendeshea kazi yake hutegemea sana juu ya vijana. Madaraka hayo makubwa sana ni juu ya vijana wa siku hizi ambao huifikia hatua ya utendaji. Kamwe hapajakuwako muda ambao matokeo makubwa jinsi hii yalitegemea juu ya kizazi cha wanadamu; basi, ni jambo kubwa kama nini kwamba yafaa vijana na wahitimu kwa ajili ya kazi kuu, ambayo Mungu aweza kuwatumia kama vyombo vyake. Muumbaji wao anayo madai juu yao ambayo ni makubwa kuliko mengine yote.KN 241.2

    Mungu ndiye aliyetoa uzima na karama zote za mwili na akili walizo nazo. Amewajalia akili nyingi, kusudi wapate kuaminiwa kazi ambayo itastahimili milele. Kwa hizo karama zake kuu hudai zikuzwe ipasavyo na kuzitumia vizuri akili na uelekevu wao wa moyo. Hakuwapa akili hizi ili waiipendeze tu kwa anasa, wala kutumiwa vibaya kwa mambo yaliyo kinyume cha mapenzi yake na majaliwa yake, bali wapate kuzitumia kuzidisha ujuzi wa kweli na mtakatifu ulimwenguni. Adai shukrani zao, kicho na upendo wao, kwa ajili ya wema wake wa daima na fadhili zake zisizo na mwisho. Adai kwa haki utii wa sheria zake na kwa kanuni zote za hekima ambazo zitawazuia na kuwalinda vijana na hila zake Shetani na kuwaongoza katika njia za amani.KN 241.3

    Ikiwa vijana wangeona kuwa kwa kuzitii sheria na amri za shule zetu wanafanya tu kile ambacho kitazidisha ubora wa cheo chao miongoni mwa watu, kukuza tabia, kuadilisha moyo, na kuzidisha mraha yao, wasingeziasi amri za haki na masharti ya halali, wala kuingia katika kuanzisha shuku na lawama juu ya shule hizo. Yafaa vijana wetu wawe na roho ya nguvu na uthabiti kuyatimiza madai juu yao, na hilo litakuwa thibitisho la kufaulu kwao. Tabia ya kishenzi na ya upotevu wa vijana wengi katika kizazi hiki cha ulimwengu hutia uchungu moyoni. Lawama nyingi ni juu ya wazazi wao nyumbani. Pasipo kicho cha Mungu hakuna awezaye kufurahi kwa kweli. 43.KN 241.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents