Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuelekea kushikwa na ugonjwa huzidishwa mara kumi kwa kula nyama. 42T 64;

    Wanyama wana ugonjwa, na kwa kuishiriki nyama yao, twapanda mbegu za ugonjwa katika minofu na damu yetu wenyewe. Ndipo tukibadilisha makao na kuwekwa mahali penye malaria, twajiona kuwa tuko hatarini zaidi; pia tukiwa mahali penye magonjwa ya kulipuka na yenye kushika watu wengi pamoja na wenye kuambukiza, mwili hauna hali ya kujikinga.KN 259.4

    Kwa nuru niliyopewa na Mungu, kuenea kwa ‘saratani’ na magonjwa mengine yanayoleta uvimbe hutokana zaidi na kula nyama kwa wingi. 5CD 386388;KN 259.5

    Mahali pengi samaki huharimishwa kwa uchafu wanaokula ambao huleta ugonjwa. Hali hiyo huonekana hasa mahali ambapo samaki hukutana na taka za kila namna za miji mikubwa. Samaki ambao wanajilisha takataka za maji hayo machafu huweza kupita mpaka kwenye maji yaliyo mbali, nao huweza kunaswa manali ambapo maji ni safi. Hivyo wakitumiwa kwa chakula huleta ugonjwa na mauti kwa wale wasiodhani kuna hatari kama hiyo.KN 259.6

    Madhara ya chakula cha nyama wakati mwingine hayawezi kubainika upesi, lakini hilo si jambo lenye kukithibitisha kuwa hakina madhara. Ni wachache wawezao kusadikishwa kwamba nyama waliyokula ndiyo ambayo imetia sumu damu yao na kuwaletea maumivu. Wengi huuawa na magonjwa ambayo hutokana hasa na kula nyama, asili yake hasa haidhaniwi nao wenyewe wala na watu wengine. 6MH 314, 315;KN 259.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents