Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nguvu kwa Njia ya Utii

    Wajibu mzito huwakalia wale wanaoijua kweli, hata matendo yao yote yatapatana na imani yao, na ya kuwa maisha yao yatasafishwa na kutakaswa nao huwa tayari kwa kazi ambayo haina budi kutendwa upesi katika siku hizi za mwisho za ujumbe huu. Hawana nafasi wala nguvu za kutumia kwa kujifurahisha kwa tamaa ya chakula. Yafaa maneno haya yatujie sasa na msukumo wa moyoni: “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana” (Matendo 3:19). Kuna wengi miongoni mwetu wenye upungufu katika mambo ya kiroho na ambao, kama wasipoongoka kabisa, yamkini watapotea. Je, mwaweza kufanya ujasiri!KN 264.1

    Mungu ataka watu wake wawe na maendeleo ya daima. Tunahitaji kufahamu kuwa tamaa mbaya ya chakula ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo bora ya akili na ya utakaso wa roho ya mtu. Kwa maungamo yetu yote ya matengenezo ya afya wengi wetu hula vibaya, isivyofaa. Kuiendekeza tamaa ya chakula ni sababu kubwa kabisa ya udhaifu wa mwilini na pia ni chanzo hasa cha udhaifu na kufa kabla ya uzee. Basi, mtu mwenye kujitahidi kuwa na usafi wa moyoni na akumbuke kuwa ndani ya Kristo kuna uwezo wa kuitawala tamaa ya chakula.KN 264.2

    Kama tungaliweza kufaidiwa na kule kuendekeza uchu wa nyama, nisingaliwatolea ombi hili; lakini najua hatuwezi kunufaika. Vyakula vya nyama hudhuru hali njema ya mwilini, nasi twapaswa kutovishiriki. Wale walio mahali wawezapo kujipatia chakula kisicho cha nyama, lakini wanaochagua kuyafuata mapenzi yao wenyewe katika jambo hili, kula na kunywa kama wapendavyo, kidogo kidogo watazidi kuwa watu wasioyajali mafundisho ambayo Bwana aliyatoa juu ya mambo mengine ya kweli ya wakati huu nao watapotewa na akili zao za kuona ukweli; yumkini watavuna walivyopanda.KN 264.3

    Nimeamriwa kwamba wanafunzi katika shule zetu wasipewe vyakula vya nyama wala vyakula visitayarishwe kwa njia zinazojulikana kuwa hazifai kwa alya. Si vizuri kitu cho chote ambacho kitaamsha kiu na vileo kuwekwa mezani. Nawasihi wazee na vijana na watu wazima. Jihinisheni vitu hivyo ambavyo huwadhuru. Mtumikieni Bwana kwa kujinyima.KN 264.4

    Kuna wengi ambao huona kuwa hawawezi kuendelea vizuri bila vyakula vya nyama; lakini ikiwa hao wangejiweka upande wa Bwana, wakiwa wamekwisha kuazimia kabisa kuenenda kadka njia anayowaongoza, wangepokea nguvu na hekima kama Danieli na wenzake. Wangeona kuwa Bwana angewapa busara nzuri.KN 265.1

    Wengi wangeshangazwa kuona kiasi ambacho kingaliweza kuwekwa akiba kwa ajili ya kazi ya Mungu kwa matendo ya kiasi. Idadi ndogo ya fedha mayopatikana kwa kujinyima itafanya makuu kwa kuijenga kazi ya Mungu kuliko ile vipaji vikubwa zaidi vinayofanya, ambavyo havikuhitaji kuwa na kiasi.KN 265.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents