Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushupavu Hudhuru Matengenezo ya Afya

    Wengine miongoni mwa watu wetu, huku wakiwa wanaacha kabisa kula vyakula vibaya, hawajali kujipatia vitu vinavyolazimu kuihifadhi afya ya mwili. Wale wanaoshupaa katika kuyafikiri haya matengenezo ya afya wako katika hatari ya kutayarisha vyakula visivyo na ladha, na visivyo na utamu hata kuwafanya wasiridhike navyo. Chakula kingetayarishwa kwa njia ambayo itakuwa venye ladha na kutia afya pia. Yafaa kisinyang’anywe kitu kile ambacho mwili wakihitaji. Natumia chumvi, na siku zote nimefanya hivyo, kwa sababu chumvi si kitu chenye madhara, bali kwa tamu kwa maziwa kidogo au mafuta yanayoganda juu ya maziwa yaliyochemswa (cream), au kwa kutumia kitu kingine cha aina hiyo.KN 268.1

    Huku maonyo yakiwa yametolewa juu ya hatari ya watoto wadogo kupatwa na ugonjwa kwa kutumia siagi, na mdhara ya kutumia mayai, lakini, haitupasi kuhesabu kuwa m uhalifu wa kanum za afya kuyatumia mayai yatokayo kwa kuku wanaotunzwa vizuri na kulishwa vizuri. Mayai yana nguvu ambazo ni zenye kuzuia sumu fulani.KN 268.2

    Wengine wakiacha kutumia maziwa, mayai na siagi, hukosa kuupatia mwili chakula cha kufaa, na hatimaye hudhoofika na kushindwa kufanya kazi. Kwa njia hiyo matengenezo ya afya hupata sifa mbaya. Kazi tuliyojaribu kuijenga kwa uthabiti inatiwa mashakani na mambo mageni ambayo Mungu hakuyataka yawepo, na nguvu za kanisa zinapoozeshwa. Lakini, Mungu ataingilia kuyazuia matokeo ya baadaye ya mawazo hayo yenye nguvu mno. Injili yapasa kuwapatanisha wanadamu wenye dhambi. Yapasa kuwakusanya pamoja matajiri na maskini miguuni mwa Yesu.KN 268.3

    Utakuja wakati ambapo yaweza kutubidi kuacha kutumia vyakula vingine tunavyotumia sasa, kama vile maziwa na mafuta yanayopatikana katika maziwa na mayai; lakini si lazima kujitwisha mashaka kwa kufanya hivyo mapema na kuzidi mno katika kutokutumia vitu vya aina hiyo sasa. Ngojeni mpaka hali ya mambo itakapolazimu kufanya hivyo na Bwana aitayarishie njia.KN 268.4

    Wale ambao watafanikiwa katika kutangaza kanuni za matengenezo ya afya hawana budi kulifanya Neno la Mungu kiongozi na mshauri wao. Kadiri tu walimu wa hizi kanuni za matengenezo ya afya wanavyofanya hivi ndivyo wawezavyo kusimama mahali pafaapo kuyakinga mashambulio. Kamwe tusitoe ushuhuda ulio kinyume cha matengenezo ya afya kwa kutotumia chakula bora, kitamu, badala ya vyakula vyenye madhara ambavyo tumevikataa. Usitie nguvu kiu ya vileo kwa njia iwayo yote. Kula tu chakula kifaacho, chepesi, kisichokolezwa kwa viungo vikali vya chakula; tena mshukuru Mungu daima kwa ajili ya kanuni za matengenezo ya afya. Kwa mambo yote uwe mwaminifu na mnyofu, nawe utapata ushindi wa thamani.KN 268.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents