Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ndipo Mungu Ataweza Kubariki

    Wale wachungaji wanaojiona wako huru kuindekeza tamaa ya chakula wana upungufu mkubwa. Mungu anataka wawe viongozi wa matengenezo ya afya. Ataka waifuate maishani mwao, nuru lliyotolewa juu ya jambo hili. Nasikitika nikiona wale ambao yawapasa wawe wenye bidii kuzishika kanuni zetu za afya, hawajaongoka bado na kuifuata njia bora ya kuishi. Naomba ili Bwana apate kuwavuta mioyoni mwao kusudi waone hasara kubwa inayowakabili. Ikiwa mambo yangekuwa kama ipasavyo nyumbani mwa watu wa makanisa yetu, tungeweza kumfanyia Bwana kazi iliyo kubwa maradufu.KN 269.2

    Kusudi kutakaswa na kudumu kuwa safi, Waadventista Wasabato hawana budi kuwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwao na nyumbani mwao, Bwana amenionyesha kwamba Israeli wa leo wakijinyenyekeza mbele yake, na kulisafisha hekalu la rohoni, na kuondoa uchafu wote, atazisikia sala zao kwa ajili ya wagonjwa, na atayabariki matumizi ya dawa zake kwa magonjwa. Kwa imani mwanadamu akifanya yote awezayo kupigana na ugonjwa, akizitumia njia nyepesi za kutibu magonjwa ambazo Mungu ametoa, jitihada zake zitabarikiwa na Mungu.KN 269.3

    Ikiwa baada ya nuru kubwa hivi kutolewa, watu wa Mungu watakuwa wakiyafurahia mazoea mabaya, wakijipendeza nafsi na kukataa kuongoka, watapatwa na madhara yanayotokana na uasi. Kama walikusudia kuiriahisha tamaa ya chakula lliyotoka kwa hali iwayo yote, Mungu hatawaokoa na madhara ya anasa zao kwa mwujiza. Watalala “kwa huzuni,” Isaya 50:11.KN 269.4

    Wengi kama nini hupotewa na mibaraka mikubwa ambayo Mungu amewawekea akiba katika afya na mibaraka ya mambo ya kiroho! Wako watu wengi wenye kujitahidi kupata ushindi wa pekee na mibaraka maalum ili wafanye makuu. Mpaka sasa huona daima kuwa yawapasa kushindana, vikali katika maombi kwa machozi. Hao nao wakiyachunguza Maandiko kwa kuomba ili kujua wazi mapenzi ya Mungu, ndipo wayatimize mapenzi yake kwa moyo wote bila kujipendeza nafsi wenyewe, watapata raha. Maumivu yote, machozi na jitihada zote, havitawaletea mbaraka ambao wanatamani kuupata. Nafsini mtu hana budi kujitoa. Yawapasa kuifanya kazi mayojitokeza yenyewe na kujitwalia kwa wingi neema ya Mungu waliyoahidiwa wote waombao kwa imani.KN 269.5

    Yesu alisema, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate” (Luka 9:23). Tumfuateni Mwokozi katika utovu wake wa anasa na kuwa na kiasi. Tumwinueni yule Mtu wa Kalwari kwa neno na kwa mwenendo mtakatifu. Mwokozi huwakaribia sana wale wanaojitoa wakfu kwa Mungu. Ikiwa palikuwapo wakati ambapo tulihitaji kazi ya Roho wa Mungu mioyoni na maishani mwetu, ni sasa. Basi na tushike sana uwezo huu mtakatifu ili tuwe na nguvu kuishi maisha matakatifu na ya kujitoa. 19T 153 - 166.KN 270.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents