Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 1 - Njozi ya Ijara ya Waaminifu

    (Njozi Yangu ya Kwanza)

    WAKATI nilipokuwa nikiomba katika chumba cha ibada nyumbani, Roho Mtakatifu alinishukia, nami nikaona kama nainuliwa juu, juu mbali na ulimwengu wa giza. Nikageuka kuwatafuta Waadventista ulimwenguni, lakmi sikuweza kuwaona, sauti iliponiambia, “Tazama tena, na tazama kidogo.” Kwa maneno haya nikainua macho yangu, nikaona njia nyembamba iliyonyoka, juu iliyoinuliwa juu ya ulimwengu. Juu ya njia hii Waadventista walikuwa wakisaflri kwenda katika mji ambao ulikuwa mbali mwisho wa njia. Walikuwa nayo nuru kubwa iliyosimikwa nyuma yao mwanzoni mwa hiyo njia, ambayo malaika aliniambia kuwa ilikuwa Kilio cha Usiku wa Manane. Nuru hii iling’aa njiani pote na kuangaza miguuni mwao kusudi wasije wakajikwaa. Waliendelea kuwa salama ili mradi tu wanadumu kuyakaza macho yao kwa Yesu ambaye alikuwa mbele yao akiwaongoza kwenda jiiim. Lakini mara wengine wakachoka, na kusema mji ulikuwa mbali sana, nao walitazamia kuwa wakati huo wangalikuwa wamekwisha kuuingia. Ndipo Yesu akawatia moyo kwa kuuinua mkono wake wa kuume wa fahari, na kutoka mikononi mwake nuru ikaja ambayo iliangaza juu ya kikosi cha Waadventista, nao wakapaza sauti, “Haleluya!” Wengine wakakanusha ile nuru nyuma yao na kusema kuwa si Mungu aliyekuwa amewaongoza mpaka napo. Nuru ile nyuma yao ikazimika, ikiiacha miguu yao gizani kabisa nao wakajikwaa na kukosa kuiona alama na Yesu, nao wakapotea njia na kushuka duniani penye giza na maovu. Mara tukaisikia sauti ya Mungu kama maii mengi, iliyotujulisha siku na saa ya kuja kwa Yesu. Watakatifu walio hai, hesabu yao 144,000 walijua na kuifahamu sauti hii, huku waovu wakifikiri llikuwa radi na tetemeko la nchi. Wakati Mungu alipotangaza wakati huo, akatumwagia Roho Mtakatifu, na nyuso zetu zikaanza kuang’azwa na kung’aa kwa utukufu wa Mungu, kama uso wa Musa ulivyong’aa aliposhuka kutoka Mlima Sinai.KN 37.1

    Wale 144,000 wote walitiwa muhuri na walikuwa na umoja kabisa. Juu ya vipaji vya nyuso zao paliandikwa, Mungu, Yerusalemu Mpya, na nyota ya fahari yenye jina jipya la Yesu. Waovu waliikasirikia hali yetu takatifu na ya furaha, nao wakaturukia kwa nguvu kutushika ili kututupa gerezani, wakati huo tulinyosha mkono katika jina la Bwana, nao wakaanguka chini wasiweze kujimudu. Kisha ikawa sinagogi la Shetani (wale waliochagua kumfuata Shetani) wakajua kuwa Mungu alikuwa ametupenda sisi ambao tuliweza kutawadhana miguu na kuwasalimu ndugu kwa busu takatifu, nao wakasujudu miguuni mwetu.KN 37.2

    Punde macho yetu yakavutwa mashariki, maana wingu dogo jeusi lilikuwa limezuka, ukubwa wake kama nusu ya kiganja cna mkono wa mtu, ambalo sote tunalijua kwamba lilikuwa ishara ya Mwana wa Adamu. Sisi sote kimya kabisa tukalikazia macho wingu lile likikaribia zaidi na kuzidi kuwa jepesi, tukufu, na la fahari zaiai, mpaka likawa wingu kubwa jeupe. Chini lilionekana kama moto; upinde wa mvua ulikuwa juu ya wingu hili huku pande zote kulizunguka palikuwa na taji nyingi Nyayo za miguu yake zilikuwa zinaonekana kama mto; katika mkono wake wa kuume alikuwa na mundu mkali; katika mkono wa kushoto, tarumbeta ya fedha. Macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, nayo yaliwachunguza watoto wake kabisa. Kisha nyuso zote zikabadilika rangi, na wale ambao Mungu amewakataa nyuso zao zikawa nyeusi. Kisha sisi sote tukapaza sauti, “Ni nani awezaye kusimama? Vazi langu ni jeupe lisilo na mawaa?” Ndipo malaika wakakoma kuimba, na pakawa na kitambo cha kimya cha ajabu, wakati Yesu aliposema: “wale wenye mikono safi na mioyo safi wataweza kusimama; Neema yangu yakutosha.” Hili likang’aza nyuso zetu, na furaha ikamjaa kila mmoja moyoni. Na wale malaika wakapiga muziki wakapaza sauti juu zaidi na kuimba tena, huku lile wingi likizidi kukaribia zaidi dunia.KN 38.1

    Ndipo tarumbeta ya Yesu ya fedha ikalia akishuka juu ya wingu, amezingirwa na ndimi za moto. Akayakodolea macho makaburi ya watakatifu waliolala, kisha akayainua macho yake na mikono mbinguni, na kupaza sauti, “Amkeni! Amkeni! Amkeni! Enyi mlalao mavumbini, ondokeni.” Ndipo pakawa na tetemeko kuu la nchi. Makaburi yakafunuka, na waiu wakatoka wamevikwa kutokufa. Wale 144,000 wakapaza sauti, “Haleluya!” wakiwatambua marafiki zao waliotengwa nao na mauti, na dakika hiyo hiyo tukabadilishwa na kunyakuliwa pamoja nao kwenda kukutana na Bwana hewani.KN 38.2

    Sote tukaingia winguni pamoja, tukapaa siku saba kwenda penye bahari ya kioo, wakati Yesu alipozileta taji, na kwa mkono wake mwenyewe wa kuume kutuvika hizo taji vichwani mwetu. Akatupa vinubi vya dhahabu na alama za ushindi. Hapa juu ya bahari ya kioo wale 144,000 walisimama mraba kamili. Wengine wao walikuwa na taji zing’aazo sana, wengine hawakuwa na zenye kung’aa namna ile. Taji zingine zilionekana kuwa nzito kwa kuwa na nyota nyingi, huku zingine zikiwa na nyota chache tu. Wote waliridhika kabisa na taji zao. Nao wote walivikwa vazi jeupe la utukufu kutoka mabegani mwao hadi chini miguuni pao. Malaika walituzunguka pande zote tukitembea juu ya bahari ya kioo kwenda langoni mwa mji. Yesu akauinua mkono wake hodari, wenye utukufu, akaushika mlango wa lulu, kurudisha nyuma juu ya bawaba zake zinazomeremeta, na kutuambia, “Mmeyafua mavazi yenu katika damu yangu, mkasimama imara kuitetea kweli yangu, ingieni.” Sote tukaingia kwa taratibu na kujiona moyoni kuwa tulikuwa na haki kamili mjini.KN 38.3

    Hapo tukauona mti wa uzima na kiti cha enzi cha Mungu. Katika kiti hiki cha enzi kukatoka mto wa maji safi, kila upande wa mto huu palikuwa na mti wa uzima. Upande mmoja wa mto huu palikuwa na shina la mti, na shina lingine tena upande wa pili wa mto, yote mawili ya dhahabu safi, yenye kupenya nuru. Kwanza nalidhani naliona miti miwili. Nikatazama tena, nikaona kuwa iliunganika juu na kuwa mti mmoja. Matawi yake yaliinama mpaka mahali tuliposimama, na matunda yalikuwa mazuri mno; yakaonekana kama dhahabu iliyochanganywa na fedha.KN 39.1

    Sote tukaenda chini ya mti huu na kuketi kuangalia utukufu wa mahali hapa, wakati ndugu Fitch na Stockman, waliokuwa wameihubiri habari njema ya ufalme, na ambao Mungu alikuwa amewalaza kaburini kuwaokoa, wakapanda, kwetu na kutuuliza kilichokuwa kimetukia walipokuwa wamelala. Tukajaribu kukumbuka taabu zetu kubwa kabisa, lakini zilionekana kuwa ndogo sana zikilinganishwa na utukufu mwingi wa milele uzidio sana ambao ulituzunguka hata hatukuweza kuzitaja, nasi wote tukapaza sauti, “Haleluya, mbinguni ni rahisi ya kutosha!” nasi tukavipiga vinubi vyetu vizuri mno na kuifanya mbingu kurudisha mwangwi.KN 39.2

    Yesu akatuongoza sote tukashuka kutoka mji ule mpaka duniani humu, juu ya mlima wa ajabu, ambao haukuweza kumstahimili Yesu, nao ukapasuka vipande vipande, pakawa na uwanda wa ajabu. Kisha tukatazama juu na kuuona ule mji mkuu, wenye misingi kumi na miwili, na milango kumi na miwili, mitatu kila upande, na malaika mmoja katika kila mlango. Sote tukapaza sauti, “Mji, mji mkuu, unakuja, unashuka kutoka kwa Mungu mbinguni,” nao ukaja na kutuama juu mahali tuliposimama. Kisha tukaanza kuvitazama vitu vya fahari nje ya mji huo. Hapo nikaona nyumba nzuri mno, zilizoonekana kama fedha, zimetegemezwa kwa nguzo nne, zilizopambwa kwa lulu nzuri mno kutazama. Hivi zilipaswa kukaliwa na watakatifu. Kila moja ilikuwa na kibao cha kutundikia ukutani cha dhahabu. Nikawaona watakatifu wengi waliingia nvumba hizi wakavua taji zao zing’aazo na kuziweka kibaoni, kisha wakaenda shambani karibu na nyumba hizo kufanya kitu na udongo; siyo kama tupaswavyo kufanya na udongo hapa; la hasha. Nuru nzuri ajabu iling’aa pande zote vichwani mwao, nao walikuwa wanaendelea kupaza sauti na kumsifu Mungu.KN 39.3

    Nikaona shamba lingine lililojaa maua ya kila namna, na nikiyachuma, nikapaza sauti, “Kamwe hayatanyauka.” Tena nikaona shamba la majani marefu, zuri sana kutazama: lilikuwa la rangi ya kijani kibichi na lilikuwa likirudisha nuru ya fedha na dhahabu likipepea kwa fahari kwenye utukufu wa Yesu Mfalme. Kisha tukaingia uwanda mmoja uliojaa wanyama wa kila aina-simba, mwana-kondoo, chui, na mbwa wa mwitu, wote pamoja katika umoja kamili. Tukapita katikati yao nao wakafuata taratibu kwa amani. Kisha tukaingia mwituni, siyo kama misitu minene tuliyo nayo hapa; la hasha; siyo yenye giza kama hapa, bali ni mizuri mno pande zake zote; matawi ya miti yaliyumba-yumba, nasi sote tukapaza sauti, “Tutakaa salama mahali hapa pakame na kulala penye misitu.” Tukapita mapori, maana tulikuwa safarini kwenda Mlima Sayuni.KN 39.4

    Tulipokuwa tukisaflri, tukakutana na kundi la watu ambao walikuwa pia wakiyakaza macho yao kutazama utukufu wa mahali pale. Nikaona rangi nyekundu kama pindo la mavazi yao; taji zao zilikuwa zenye kung’aa; mavazi yao yalikuwa safi meupe. Akasema walikuwa wafia dini (watu waliouawa kwa sababu ya kukataa kuikana imani yao) ambao walikuwa wameuawa kwa ajili yake. Pamoja nao palikuwako kundi la watoto wengi mno. Wao pia walikuwa na pindo la rangi nyekundu juu ya mavazi yao. Mlima Sayuni ulikuwa mbele yetu, na juu ya mlima palikuwako na hekalu zuri mno, na pande zote kuuzunguka palikuwa na milima mingine saba, ambayo juu yake palisitawi wandi na maua mazuri jamii ya yungiyungi. Nami nikawaona watoto wakipanda, au kama walichagua kufanya hivyo, walitumia mabawa yao madogo na kuruka, mpaka juu ya kilele cha milima hii na kuchuma maua ambayo kamwe hayanyauki. Palikuwa na miti ya kila aina pande zote kulizunguka lile hekalu kupapamba mahali hapo: namna ya mti mweupe mgumu (box), msunobari (pine), mwerezi, mfuta (the oil) namna ya mti mdogo (the myrtle), mkomamanga, na mtini uliinama chini kwa uzito wa tini zake za majira ya kufaa hii ilipafanya mahali hapa kuwa pazuri mno pande zote. Na tulipokuwa karibu kuingia hekalu takatifu, Yesu akipaza sauti yake tamu na kusema, “Wale tuKN 40.1

    144,0 ndio wenye kuingia mahali hapa,” nasi tukapaza sauti, “Haleluya.”KN 40.2

    Hekalu hili lilitegemezwa na nguzo saba, zote za dhahabu ipenyayo nuru, zimepambwa na lulu nzuri mno. Vitu vya ajabu nilivyoviona hapo siwezi kuvielezea. Ah, laiti ningeweza kusimulia kidogo juu ya utukufu wa ulimwengu ule mzuri zaidi. Nikaona pale vibao vya mawe ambamo majina ya wale 144,000 yaliandikwa kwa herufi za dhahabu. Tulipokuwa tumekwisha kuutazama utukufu wa lile hekalu, tukatoka, naye Yesu akatuacha na kwenda mjini. Mara tukaisikia sauti yake tamu tena, akisema, “Njoni, watu wangu, mmetoka katika dhiki ile iliyo kuu, na mmefanya mapenzi yangu; mkateseka kwa ajili yangu; njoni chakulani, maana nitajifunga, na kuwahudumia.” Tukapaza sauti, “Haleluya! Utukufu!” na kuingia mjini. Nami nikaona meza ya fedha safi; ilikuwa ndefu maili nyingi, walakini macho yetu yaliweza kuiona mpaka mwisho. Nikaona matunda ya mti wa uzima, mana, malozi, tini, makongamanga, zabibu, na matunda ya aina nyingi nyingine. Nikamwuliza Yesu kuniruhusu niyale matunda hayo. Akasema. “Siyo sasa. Wale wanaokula matunda ya nchi hii nawarudi tena duniani. Lakini muda kitambo, kama ukiwa mwaminifu, utakula matunda ya mti wa uzima na kunywa maji ya chemchemi.” Naye akaniambia, “Huna budi kurudi duniani tena na kuwasimulia wengine mambo ambayo nimekufunulia.” Kisha malaika akanichukua chini taratibu mpaka katika ulimwengu huu wa giza. Wakati mwingine nafikiri siwezi kukaa hapa tena; vitu vyote vya dunia huonekana kuwa vibaya vya kutia huzuni sana. Najiona hali ya upweke sana hapa, maana nimeona nchi nzuri zaidi. Ah, laiti ningekuwa na mabawa kama njiwa, ndipo ningeruka mbali na kuwa katika raha!. (Early Writings, uk. 14-20).KN 40.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents