Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 2 - Wakati Wa Mwisho

    TUNAISHI katika wakati wa mwisho. Dalili za nyakati hizi zinazotimia haraka hutangaza kuwa kuja kwa Kristo kumekaribia. Siku tunazoishi ni nyeti na za muhimu. Roho wa Mungu anaondolewa duniani, taratibu, lakini kwa hakika. Mapigo na hukumu tayari vinawaangukia wenye kuidharau neema ya Mungu. Misiba mikubwa katika nchi kavu na baharini, hali ya machafuko ya watu, habari za hatari za vita, ni za kuogofya. Haya yanaashiria matukio yanayokaribia ya mambo makubwa. Nguvu za uovu zinaungana na kujizatiti. Wanakusanya nguvu kwa ajili ya hatari kuu za mwisho. Mabadiliko makubwa hayana budi kutokea ulimwenguni mwetu siku si nyingi, na mabadiliko ya mwisho yatakuwa ya haraka haraka. Hali ya mambo ulimwenguni huonyesha kuwa nyakati za dhiki zinatukabili. Magazeti ya kila siku yamejaa mambo yanayoonyesha vita kali muda si mrefu ujao. Uporaji wa hadharani unatokea mara kwa mara. Migomo ni jambo la kawaida. Wizi na uuaji hufanywa kila upande. Watu makatili wanawaua watu, wanaume, wanawake, na watoto wadogo. Watu wamepumbazishwa na muovu, na kila aina ya uovu imeenea po pote.KN 42.1

    Adui amefaulu katika kupotosha haki na katika kuijaza mioyo ya watu tamaa ya kujipatia mali isiyo ya halali. “Haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia” (Isaya 59:14). Katika miji mikuu wako wengi wanaoishi katika nali ya umaskini na ufukara, karibia kabisa kukosa chakula, nyumba, na nguo; huku katika miji hiyo hiyo wakiwapo wale ambao wanacho kila kitu wanachotamani, wenve kuishi kitajiri, na kujipendeza kwa anasa, wakitumia pesa zao katika nyumba za kitajiri, mapambo ya mwili, au jambo lililo baya zaidi, kwa kujipendeza kwa tamaa mbaya za mwili, kwa pombe, tumbako, na vitu vingine vinavyodhuru nguvu za ubongo, na kuduwaza akili, na kuharibu moyo. Vilio vya watu wanaoumia kwa njaa vinapanda juu mbele za Mungu, huku kwa udhalimu wa kila aina na ukandamizaji watu wanajilundikia mali nyingi.KN 42.2

    Katika tukio moja nikiwa kwenye jiji la New York, majira ya usiku nilionyeshwa majengo yakipanda ghorofa moja baada ya nyingine kuilekea mbingu. Majengo haya yalishuhudiwa kitaalam kuwa imara yasiyoweza kushika moto; na yalijengwa kuwatukuza wenye kuyamiliki na wajenzi. Majengo haya yakazidi kuinuka juu, nayo yalijengwa kwa kutumia vifaa vya gharama kubwa sana. Wale wamiliki wa majengo haya hawakujiuliza: “Twawezaje kumtukuza Mungu vizuri zaidi?” Hawakumwaza Mungu. Kadiri majengo haya marefu yalivyopanda juu, wamiliki wake walifurahi huku wakijazwa na tamaa ya kutaka makuu kwamba walikuwa na fedha ya kutumia katika kujitukuza nafsi zao na kuchochea wivu kwa maiirani zao. Fedha iliyo nyingi ambayo wameitumia kwa njia nii imepatikana kwa udnalimu, kwa kuwaonea maskini. Wamesahau kuwa mbinguni huandikwa habari za kila tendo; kila jambo lisilo la haki, kila udanganyifu, huandikwa pale. Maono mengine niliyoonyeshwa yalikuwa kelele ya dharura ya kujulisha watu hatari ya moto. Watu wakayatazama yale majengo marefu yaliyodhaniwa kuwa hayawezi kuungua moto na kusema: “Yako salama kabisa.” Lakini majengo haya yaliteketea kana kwamba yalikuwa yamejengwa kwa lami. Mashine za kuzimia moto hazikuweza kufanya cho chote kuzuia uharibifu huo. Zima moto walishindwa kabisa kutumia mashine hizo.KN 42.3

    Nimeamriwa kuwa saa ya Bwana ifikapo, ikiwa hakuna mabadiliko yaliyofanyika katika mioyo yenye kiburi na majivuno, na ya wenye kutaka makuu, watu wataona kuwa mkono ule ambao ulikuwa na nguvu kuokoa utakuwa wenye nguvu kuangamiza. Hakuna nguvu duniani iwezayo kuuzuia mkono wa Mungu. Wala hakuna vifaa viwezavyo kutumiwa katika kujenga majengo ambavyo vitayalinda yasiharibiwe saa ya Mungu iliyowekwa ifikapo kuwapatiliza watu uasi wao juu ya Sheria yake na kujitakia makuu. Si wengi, hata miongoni mwa wataalamu na wakuu wa nchi wanaofahamu asili ya hali lliyoko sasa miongoni mwa jamii za watu. Wale wanaotawala serikalini hawawezi kutatua tatizo la kuharibika kwa tabia za watu, umaskini, ufukara, na kuongezeka kwa uhalifu wa sheria. Wanasumbuka bure kuweka sheria za kutenda kazi za biashara kwa njia ya salama zaidi. Kama wangeyatii mafundisho ya Neno la Mangu, wangepata jawabu la marumbo yanayowatatiza.KN 43.1

    Maandiko Matakatifu huelezea hali ya ulimwengu karibia na Kuja kwa Kristo Mara ya Pili. Juu ya watu ambao kwa unyang’anyi na kutaka bei kubwa kwa vitu wanalundika mali nyingi, imeandikwa: “Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelel, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmefanya anasa katika dunia, nakujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.” (Yakobo 5:3-6).KN 43.2

    Lakini nani asomaye maonyo yaliyotolewa na dalili hizi zenye kutimia haraka za nyakati hizi? Walimwengu wanazionaje moyoni? Badiliko gani huonekana moyoni mwao? Hakuna zaidi ila moyo ule ule ulioonekana katika watu wa ulimwengu wa kale, siku za Nuhu. Kwa kushughulika sana na biashara na anasa, hata kutofikiri vingine, watu wale walioishi kabla ya gharika “wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote,’ (Mathayo 24:39). Walikuwa na maonyo yaliyotumwa kutoka mbinguni, lakini walikataa kusikiliza. Leo vile vile walimwengu hawajali hata kidogo sauti ya Mungu ya onyo. wanakwenda mbio penye uharibifu wa milele. Ulimwengu unastushwa na roho ya vita. Unabii wa sura ya kumi na moja wa Danieli karibu umefikia utimizo wake kabisa. Siku si nyingi maono ya dhiki iliyotajwa katika unabii huo yatatokea.KN 43.3

    “Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake Kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa wame-teketea, watu waliosalia wakawa wachache tu Sauti ya furaha ya kinubi inakoma” (Isaya 24:1-8). “Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi” (Yoeli 1:15).KN 44.1

    “Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. Nikaangalia na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka” (Yeremia 4:23-26). “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo; maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo” (Yeremia 30:7).KN 44.2

    Si wote ulimwenguni humu waliomwasi Mungu na kumfuata yule adui. Si wote waliochagua kutokumtii Mungu. Wako wachache walio waaminifu kwa Mungu; maana Yohana aandika: “Hapo ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu” (Ufunuo 14:12). Karibu kutakuwa vita kali baina ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia. Bado kitambo kidogo kila kitu kiwezacho kupepetwa kitapepetwa, ili vitu visivyoweza kupepetwa visalie.KN 44.3

    Shetani ni mwanafunzi wa Biblia mwenye bidii. Anajua kuwa muda wake ni mfupi, naye anatafuta katika kila jambo kuzuia kazi ya Mungu duniani. Ni jambo lisilowezekana kutoa wazo lo lote kuhusu uzoefu wa watu wa Mungu ambao watakuwa hai duniani wakati utukufu wa mbinguni na kurudiwa kwa mateso ya zamani vitakapochangamana. Watatembea katika nuru itokayo kitini pa enzi pa Mungu. Kwa njia ya malaika daima kutakuwa na mawasiliano baina ya Mungu mbinguni na watu wake duniani. Naye Shetani, akizungukwa na malaika wabaya, na kujifanya kuwa yeye ni Mungu, atafanya miujiza ya kila namna, kuwadanganya yumkini, hata wateule. Usalama wa Watu wa Mungu hautapatikana katika kufanya miujiza, maana Shetani ataiga miujiza ltakayofanywa. Wakati wakishitakiwa na wakati wakijaribiwa, Watu wa Mungu watajipatia uwezo wa kusimama imara kutoka katika ishara iliyosemwa habari zake katika Kutoka 31:12-18. Yawapasa kuliamini Neno lenye uzima: “Imeandikwa.” Huu ndio msingi tu ambao juu yake wanaweza kusimama salama. Wale ambao wamevunja agano lao na Mungu siku ile watakuwa hawana Mungu wala matumaini.KN 44.4

    Wenye kumwabudu Mungu watatambuliwa kwa kuiheshimu kwao amri ya nne, kwa kuwa hii ni ishara ya uwezo wa Mungu wa kuumba na ushuhuda wa madai yake juu ya kuheshimiwa na wanadamu. Waovu watabainika kwa jitihadi zao za kuvunja ukumbusho wa Muumbaji na kutukuza kile kilichoanzishwa na Rumi. Mwisho wa vita hii jamii ya Wakristo wote watagawanyika katika aina mbili kuu, wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomwabudu yule mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake. Ijapokuwa kanisa na serikali vitaunganisha nguvu zao kuwashurutisna wote, “wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,” kupokea chapa ya mnyama, walakini watu wa Mungu hawataipokea (Ufunuo 13:16). Nabii wa Patmo anaona “wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na chapa yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu,” wakiimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana-Kondoo (Ufunuo 15:2).KN 45.1

    Majaribio na taabu za kutisha sana zinawangojea watu wa Mungu. Roho ya vita inayachochea mataifa kutoka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili. Lakini katikati ya wakati huo wa dhiki ijayo,-wakati wa taabu ambayo mfano wake haujakuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati huo,-wateule wa Mungu watasimama imara. Snetani na jeshi lake hawawezi kuwangamiza maana malaika wanaowazidi nguvu watawalinda (9T 11 - 17).KN 45.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents