Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mambo Halisi Yaonyeshayo Utakaso

    Mwokozi wetu alikuwa nuru ya ulimwengu, lakini ulimwengu haukumtambua. Daima alitumika katika kazi za rehema, akitoa nuru katika njia ya wote; lakini hakuwaita wale walioingiliana naye kutazama maadili yake yasiyo na kifani, kujikana nafsi kwake, kujinyima, na wema wake. Wayahudi hawakuyasifu maisha ya namna hii. Waliihesabu dini yake kuwa isiyo na maana, kwa sababu haikupatana na kipimo chao cha uchaji wa Mungu. Wakaamua kuwa Kristo hakuwa mtu wa dini katika moyo au tabia; maana dini yao ilikuwa ya kutakabari, katika kusali hadharani mwa watu, na katika kufanya matendo ya kupenda wengine na kuwafadhili.KN 60.1

    Tunda la thamani iliyo kuu la utakaso ni sifa njema ya upole. Uzuri huu ukitawala rohoni mwa mtu, tabia hufanyizwa kwa mvuto wake. Ndipo huwapo daima kumngojea Mungu na kuitiisha nia chini ya nia yake.KN 60.2

    Kujikana nafsi, kujitoa dhabihu, wema fadhili, upendo uvumilivu, uhodari, na matumaini ya Mkristo ni matunda ya kila siku yazaliwayo na wale ambao wanahusiana kwa kweli na Mungu. Yawezekana matendo vao yasitangazwe kwa walimwengu, lakini wao wenyewe kila siku wanashindana na mwovu, na kujipatia ushindi wa thamani kuu juu ya majaribu na mabaya. Ahadi nzito hufanywa upya, na kutimizwa kwa nguvu zinazopatikana kwa kuomba kwa bidii na kukesha daima. Mwenye shauku haoni mashindano ya hawa watenda kazi walio kimya lakini jicho lake Yeye ambaye huona siri za moyoni, huona na kukubali kila jitihada itolewayo kwa unyenyekevu na upole. Sharti kupitia saa ya kujaribiwa ili kudhihirisha dhahabu safi ya upendo na imani katika tabia. Taabu na mashaka yanapolipata kanisa, ndipo bidii zisizolegea na upendo mkubwa wa wafuasi wa kweli wa Kristo hukuzwa.KN 60.3

    Wote wanaoingia katika milki yake (mtu wa kweli wa dini) hutambua uzuri na harufu nzuri ya maisha yake ya Kikristo, hali yeye mwenyewe hafahamu, maana hupatana na mazoea yake na maelekeo yake. Huomba kwa ajili ya nuru ya mbinguni, na hupenda kuenenda katika nuru hiyo. Ni chakula na kinywaji chake kuyafanya mapenzi ya Baba yake aliye mbinguni. Uhai wake umefichwa na Kristo ndani ya Mungu; lakini hajisifu kwa hili, wala haonekani kulitambua. Mungu hufurahia wanyenyekevu na wenye kujidhili ambao hufuata kabisa nyayo za Bwana. Malaika huvutwa kwao, na hupenda kukaa muda mrefu njiani mwao. Wanaweza kupitwa kando kama wasiostahili kutambuliwa na wale ambao hujikweza na wenye kuyatukuza matendo yao mema, lakini malaika wa mbinguni huinama kwa upendo juu yao nao ni kama boma la moto kuwazunguka. 7SL 11-15;KN 60.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents