Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Danieli-Kielelezo cha Maisha Matakatifu

    Maisha ya Danieli ni kielezo kilichovuviwa cha mambo yanayofanya tabia kuwa takatifu. Yanatoa fundisho kwa wote, na hasa kwa vijana. Msimamo mkali katika kupatana kabisa na matakwa ya Mungu ni wa manufaa kwa afya ya mwili na akili. Ili kuufikia upeo wa tabia ya moyoni na wa mafanikia ya kiakili, ni lazima kutafuta hekima na nguvu kutoka kwa Mungu na kuwa na kiasi katika mazoea yote ya maisha. 8SL 23;KN 61.1

    Kadiri tabia ya Danieli ilivyozidi kuwa isiyo na lawama, ndivyo chuki ilivyozidi kuamshwa juu yake na adui zake. Walijawa na hasira hata kupotewa na akili, kwa sababu hawakuweza kupata neno katika tabia yake ya moyoni au katika namna yake ya kufanya kazi zake la kuwafanya wamnung’unikie. “Ndipo wale wakasema, hatutapata sababu ya kumshtaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.” (Danieli 6:5).KN 61.2

    Fundisho kubwa kama nini limetolewa hapa kwa ajili ya Wakristo wote. Macho makali ya wivu yalikazwa kwa Danieli siku kwa siku; kutazama kwao kulitiwa makali na chuki; lakini hakuna neno wala tendo waliloweza kulihesabu kuwa kosa. Na hata hivyo hakujidai kutakaswa, bali alifanya kile kilicho bora sana-aliishi maisha ya uaminifu na ya kujitoa wakfu.KN 61.3

    Amri inatolewa na mfalme. Danieli afahamu kusudi la maadui zake kumwangamiza. Lakini habadili njia yake hata kwa jambo moja. Kwa utulivu anafanya kazi zake alivyozoea, na saa ya kusali anaenda chumbani mwake, na madirisha yake yakiwa yamefunguka wazi kuelekea upande wa Yerusalemu, anaomba dua zake kwa Mungu wa mbinguni. Kwa njia yake hii ya kutenda mambo alionyesha kwa ujasiri kuwa hakuna mamlaka yo yote ya kidunia yenye haki kuingilia baina yake na Mungu wake na kumwambia nam wa kumwomba ama nani wa kutokumwomba. Mwangalieni huyu mtu mwenye cheo kikubwa anayeishi kulingana na kanuni za Mungu! Anasimama mbele ya walimwengu leo kama kielelezo cha ujasiri wa Kikristo na uaminifu. Anamgeukia Mungu kwa moyo wake wote, ijapokuwa anajua kuwa mauti ndiyo adhabu ya uchaji wake kwa Mungu. “Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.” (Fungu 16).KN 61.4

    Asubuhi mapema mfalme akaenda haraka kwenye lile tundu la simba, akalia, “Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?” (Fungu 20). Sauti ya nabii huyu ikasikika akijibu, “Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako Ee mfalme, sikukosa neno. “Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.” (Mafungu 22, 23). Hivyo ndivyo mtumishi wa Mungu alivyookolewa. Na mtego ambao adui zake walimwekea ili kumwangamiza ukawaangamiza wao wenyewe. Kwa amri ya mfalme walitupwa tunduni, na mara hiyo wakaliwa na wale wanyama wakali.KN 62.1

    Wakati ulipokaribia mwisho wa ile miaka sabini ya utumwa akili za Danieli ziliwaza sana juu ya maneno ya unabii wa Yeremia. Danieli hautangazi uaminifu wake mwenyewe mbele za Mungu. Badala ya kujidai kuwa safi na mtakatifu, huyu nabii aliyetukuka kwa unyenyekevu alijifananisha na Israeli wenye dhambi hasa. Hekima ambayo Mungu alikuwa amempa ilikuwa kubwa sana kushinda hekima ya wakuu wa ulimwengu huu kama nuru ya jua ing’aayo mbingum adhuhuri ilivyo zaidi ya nyota hafifu sana. Hebu fikiria juu sala kutoka midomoni mwa mtu huyu mwenye kupendwa sana na Mbingu. Kwa unyenyekevu wa moyo, na kwa machozi na moyo ulioraruka, anajiombea na kuwaombea watu wa taifa lake. Anaufunua moyo wake wazi mbele za Mungu akiungama kutokustahili kwake mwenyewe na kukiri ukuu wa Mungu na adhama yake.KN 62.2

    Huku sala ya Danieli ikiendelea, malaika Gabrieli anakuja haraka kutoka mbinguni kumwambia kuwa maombi yake yamesikiwa na kujibiwa. Huyu malaika mkuu ameamriwa kumpa akili na ufahamu kumfiinulia siri za zama zijazo. Hivyo akiwa katika kutafuta kwa bidii kujua na kuufahamu ukweli, Danieli aliingizwa katika kushirikiana na mjumbe wa Mungu.KN 62.3

    atika jibu la ombi lake, Danieli hakupokea tu nuru na kweli ambayo yeye na watu wake walihitaji sana, bali maono ya mambo makuu ya wakati ujao, hata kuja kwa Mkombozi wa ulimwengu. Wale wanaojidai kuwa watakatifu, huku wakiwa hawana shauku ya kuyachunguza Maandiko Matakatifu au kushindana na Mungu katika maombi ili kupata ufahamu dhahiri zaidi wa ukweli wa Biblia, hawaujui utakaso wa kweli.KN 62.4

    Danieli alizungumza na Mungu. Mbingu zilifunuliwa mbele yake. Lakini heshima kuu aliyopewa ilikuwa asili ya unyenyekevu na kumtafuta Mungu kwa bidii. Wote wanaoamini kwa moyo neon la Mungu wataona njaa na kiu ya kuyajua mapenzi yake. Mungu ndiye asili ya kweli. Hutia nuru akili zilizoingia giza na huutia moyo wa mwanadamu uwezo wa kushika na kufahamu maneno ya kweli ambayo ameyafunua.KN 62.5

    Maneno makuu ya kweli yaliyofunuliwa na Mkombozi wa ulimwengu yanawahusu wale wenye kuitafuta kweli kama hazina iliyositirika. Danieli alikuwa mzee. Maisha vake yalikuwa yamepitia katikati ya mivuto ya jumbani mwa mfaime mkafiri, akili zake zilisumbuliwa na mambo ya dola kuu. Lakini anacha haya yote ili kuitesa roho yake mbele za Mungu, na kutafuta kujua makusudi ya Mwenyezi Mungu. Na kwa kuyajibu maombi yake, nuru itokayo mbinguni ilipelekwa kwa ajili ya wale ambao wangeishi siku za baadaye. Basi, kwa moyo wa bidii kama nini tungemtafuta Mungu, kusudi azifunue akili zetu kuyafahamu maneno ya kweli tuliyoletewa kutoka mbinguni.KN 63.1

    Danieli alikuwa mtumishi wa Mungu aliyejitoa wakfu. Maisha yake ya siku nyingi yalijawa na matendo memaya utumishi mzuri kwa Bwana wake. Usafi wake wa tabia na uthabiti wake vilikuwa sawa tu na unyenyekevu wake wa moyo na masikitiko yake mbele za Mungu kwa ajili ya makosa. Tunarudia, Maisha ya Daniel ni kielelezo kilichovuviwa cha utakaso wa kweli. 9SL 42-52;KN 63.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents