Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mahali kwa Kila Mmoja wa Watu Majumbani

    Wanawake na wanaume wanaweza kutwaa mahali pao katika kazi hii wakati wa hatari, na Mungu atafanya kazi kwa njia yao. Kama wamejazwa moyoni ujuzi wa wajibu wao, na kufanya kazi chini ya mvuto wa Roho wa Mungu watakuwa na utulivu ambao hasa hutakikana wakati huu. Mwokozi atatoa kwa wale wanawake wenve kujinyima nuru ya uso wake, na hii itawapa uwezo ambao utasninda ule wa wanaume. Wanaweza kufanya katika watu wa majumbani kazi ambayo wanaume hawawezi kufanya, kazi ambayo huyafikia maisha ya moyoni kwa ndani zaidi. Wanaweza kuikaribia mioyo ya wale ambao wanaume hawawezi kuifikia. Kazi yao inahitajika. Wanawake wenye busara na wanyenyekevu huweza kufanya kazi iliyo njema katika kueleza ukweli kwa watu majumbani mwao. Neno la Mungu lenye kuelezwa namna hii litatenda kazi yake ya kutia chachu, na kwa njia ya mvuto wake wote wa nyumbani wataongoka. 139T 128;KN 70.1

    Wote waweza kufanya kitu. Katika kujaribu kutoa udhuru, wengine husema: “Kazi za nyumbani mwangu, watoto wangu, hudai wakati wangu na mali zangu.” Wazazi, watoto wenu wangekuwa msaada kwenu, wakiongeza uwezo wenu kumtumikia Bwana. Watoto ni watu walio wadogo katika jamaa ya Mungu. Yawapasa kufundishwa kuwa uwezo wao wote wa mwili, akili, na moyo ni vyake Mungu. Wangefundishwa kusaidia katika kazi za namna mbalimbali za kufikiria wengine kuliko nafsi zao wenyewe. Usikubali watoto wako kuwa vikwazo. Yawapasa watoto kushiriki pamoja nawe mizigo ya kiroho na ya kimwili pia. Kwa kuwasaidia wengine wanaongeza furaha yao wenyewe na manufaa. 147T63;KN 70.2

    Kazi yetu kwa ajili ya Kristo haina budi kuanzia kwa watu wa nyumbam. Mafundisho ya vijana yanapasa kuwa tofauti na yale yaliyotolewa wakati uliopita. Hali yao njema hudai kazi zaidi kuliko ilivyofanywa kwao. Hakuna kazi ya muhimu kupita hiyo kwa upande wa wanawake. Kwa mafundisho na kielelezo yawapasa wazazi kuwafundisha watoto wao kuwafanyia kazi watu wasioongoka. Yawapasa watoto kufundishwa hata wawahurumie wazee na wale wanaosumbuka nao watatafuta kupunguza maumivu ya maskini na wenye taabu. Yawapasa kufundishwa kuwa wenye bidii katika kazi ya utume; na tangu utotoni kujikana nafsi na kujinyima kwa ajili ya kuwanufaisha wengine na kuendeleza kazi ya Kristo kungefundishwa, kusudi wapate kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu. 156T 429;KN 70.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents