Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuwa Mashahidi kwa Kuhamia Mahali Papya

    Si kusudi la Mungu kuwa watu wake wakae mahali pamoja jamii kubwa. Wanafunzi wa Kristo ni mawakili wake duniani, na Mungu anakusudia kuwa watawanyike pande zote nchini, katika miji mikubwa na midogo, na vijijim, kama mianga katikati ya giza la ulimwengu. Wanapaswa kufanya kazi ya utume kwa ajili ya Mungu, kwa imani na matendo yao wakishuhudia kukaribia kuja kwa Mwokozi.KN 71.1

    Washiriki wa makanisa yetu waweza kufanya kazi ambayo bado hawajaanza kuifanya ila kwa shida. Pasiwepo na watu wanaohamia mahali papya kwa ajili ya manufaa ya kiaunia tu; bali pakiwapo na mlango wa kupata maishilio, hebu jamaa walio imara katika Neno la Mungu waingie, watu wa nyumba moja au mbili mahali pamoja, kufanya kazi ya utume. Yawapasa kuona moyoni upendo kwa ajili ya roho za watu, mzigo wa kazi kwa ajili yao, na yawapasa kulifanya kuwa jambo la kujifunza jinsi ya kuwaleta kwenye ukweli. Wanaweza kugawanya vitabu na magazeti yetu, kufanya mikutano nyumbani mwao, kujua habari za majirani zao, na kuwaalika kuja katika mikutano hii. Hivyo ndivyo wawezavyo kuacha nuru yao kuangaza kwa matendo mema.KN 71.2

    Hebu watenda kazi wasimame wenyewe kwa Mungu, wakilia, wakiomba, wakifanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzao. Kumbukeni kuwa mnakimbia katika shindano, mkishindania taji ya milele. Huku wengi wakipenda sifa za watu zaidi ya kupata kibali kwa Mungu, fungu lenu na liwe kufanya kazi kwa moyo mnyenyekevu. Jifunzem kutumia imani katika kuwaweka majirani zenu mbele ya kiti cha neema na kumwomba Mungu kuigusa mioyo yao. Kwa njia hii kazi ya utume yenye matokeo mema yaweza kutendeka. Wengine waweza kufikiwa ambao wasingependa kusikiliza mhubiri au mwinjilisti wa vitabu. Na wale wanaofanya kazi kwa njia hii mahali papya watajifunza njia bora sana za kuwaendea watu na huweza kutayarisha njia kwa ajili ya watenda kazi wengine. 168T 244, 245;KN 71.3

    Watembeleeni majirani zenu na kuwaonyesha kuwa mnajali wokovu wa roho zao. Amsheni nguvu zote za kiroho zifanye kazi. Waambieni mnaowaamkia ya kwamba mwisho wa vyote umekaribia. Bwana Yesu Kristo atafungua mlango wa mioyo yao na kuamsha mioyoni mwao shauku isiyokoma.KN 71.4

    Hata wanaposhughulika na kazi zao za kila siku, watu wa Mungu waweza kuwaongoza wengine kwa Kristo. Na wakiwa katika kufanya hili watakuwa wanayo ahadi ya thamani kwamba Kristo atawapa maneno ya kusema ambayo yatawaburudisha na kuwatia nguvu maskini, wenye kusumbuka ambao wamo gizani. Imani yao wenyewe itatiwa nguvu wakifahamu kuwa ahadi ya Mkombozi matimizwa. Licha ya kuwa mbaraka kwa wengine, hata kazi waifanyayo kwa ajili ya Kristo huwaletea mbaraka wao wenyewe.KN 71.5

    Kazi kubwa yaweza kutendwa kwa kuwafundisha watu Biblia kama inavyosomeka tu. Pelekeni Neno la Mungu kwa mlango wa kila mtu, sisitizeni maneno yake yaliyo dhahiri kwenye dhamiri ya kila mtu, waambieni tena wote agizo la Mwokozi: “Mwayachunguza Maandiko” (Yohana 5:39). Waonyeni kuichukua Biblia kama ilivyo, kuomba sana hekima ya Mungu, na kisha, nuru ikiangaza, kupokea kwa furaha kila mwonzi wa thamani na kwa ujasiri kustahimili matokeo yake ya baadaye. 185T 388;KN 72.1

    Miongoni mwa washiriki wa makanisa yetu yapasa pawepo na kazi zaidi ya kwenda nyumba kwa nyumba kutoa masomo ya Biblia na kugawanya vitabu na magazeti. Tabia ya Kikristo yaweza tu kufanyika sawa sawa na kwa ukamilifu mtu anapohesabu kuwa ni majaliwa kufanya kazi pasipo kutaka kujinufaisha mwenyewe katika kulihubiri Neno la Mungu na kuisaidia kazi ya Mungu kwa fedha. Hatuna budi kupanda mbegu kando ya maji yote, kuzikabidhi roho zetu katika upendo wa Mungu, kufanya kazi maadamu ni mchana, na kutumia njia zote tulizopewa na Mungu kufanya kazi yo yote ifuatayo. Lo lote mikono yetu ipatalo kulifanya, yatupasa tulifanye kwa uaminifu; dhabihu lwayo yote tutakiwayo kutoa, yatupasa kuitoa kwa moyo mkunjufu. Kadiri tunavyopanda mbegu kando ya maji yote tutaona kuwa “apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu” (2 Wakorintho 9:6).KN 72.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents