Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 8 - Mimi Hapa, Nitume Mimi

    MWISHO u karibu, unatunyemelea, pasipo kuonekana, kama kunyatia kwa mwizi usiku. Mungu atujalie lli tusilale tena kama wengine wafanyavyo, bali tupate kukesha na kuwa na kiasi. Siku si nyingi Neno la Mungu litakuwa halina budi kushinda vizuri mno na wote ambao sasa wanachagua kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu watashinda pamoja nalo. Muda ni mfupi; usiku waja ambapo mtu hawezi kufanya kazi. Hebu wale wanaofurahi katika nuru ya Neno la kweli la wakati huu, sasa waharakishe kuwapa wengine ukweli. Bwana anauliza, “Nimtume nani?” Wale wapendao kujinyima kwa ajili ya Neno la Mungu, wanapaswa, sasa kuitikia, “Mimi hapa, nitume.”KN 74.1

    Tumefanya sehemu ndogo tu ya kazi ya kuhubiri Injili ambayo Mungu anataka sana tuifanye miongoni mwa majirani na maratiki zetu. Katika kila mji wa nchi hii yetu wako wale ambao hawajui ukweli. Na nje ya nchi yetu, ng’ambo ya bahari katika ulimwengu huu mkubwa kuna mahali pengi papya pa kazi ambapo yatupasa kuulima udongo na kupanda mbegu. 1An Appeal to Ministers and Church Officers ;KN 74.2

    Tuko karibu sana na wakati wa taabu na mashaka ambayo hayajafikiriwa na mtu ye yote bado. Uwezo utokao upande wa chini huwaongoza wanadamu vitani kinyume cha Mungu. Wanadamu wamefanya shauri moja na malaika wabaya kuitangua sheria ya Mungu. Walimwengu wanafanana na watu wa ulimwengu wa siku za Nuhu, ambao walikumbwa na Gharika, na kama watu wa Sodoma, ambao waliteketezwa kwa moto kutoka mbinguni. Nguvu za Shetani zinafanya kazi kupotosha akili za watu kutoka katika mambo ya hakika ya milele. Yule adui amepanga mambo yafae makusudi yake mwenyewe. Shughuli za kidunia, michezo, mitindo ya kisasamambo haya hushughulisha akili za watu wanaume kwa wanawake. Michezo ya furaha na masomo yasiyo na faida huharibu busara. Katika ile njia pana iendayo katika uharibifu wa milele pana maandamano makubwa. Ulimwengu, ukijawa na jeuri, karamu za furaha nyingi, na ulevi, unalibadilisha kanisa. Sheria ya Mungu, kipimo kitakatifu cha haki, inatangazwa kuwa isiyo na maana. 2 9742, 43;KN 74.3

    Je yatupasa kungoja mpaka kutimizwa kwa maneno ya unabii wa mwisho kabla ya kusema lo lote juu yao? Basi maneno yetu yatakuwa na faida gani? Tungoje mpaka nukumu za Mungu zimwangukie mkosaji kabla hatujamwambia jinsi ya kuziepuka. Iko wapi imani yetu katika Neno la Mungu? Je lazima tuone mambo yahyotabiriwa yakitimia kabla hatujaamini kile alichosema? Kwa mionzi dhahiri, nuru imetujia, ikituonyesha kuwa siku kuu ya Bwana imekaribia, ” naam I milangoni.” Hebu tusome na kufahamu kabla hatujachelewa. 3 9720;KN 74.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents