Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 12 - Kuishi Ulimwenguni Bila Kuwa Mtu wa Ulimwengu Huu

    NALIONYESHWA hatari yetu, kama watu, ya kufanana na walimwengu badala ya kufanana na Kristo. Tuko sasa mipakani mwa ulimwengu wa milele, lakini kusudi la yule adui wa roho za watu ni kuuahirishia mbali wakati wa mwisho. Shetani atawashambulia kwa kila njia aonayo yafaa wale wanaodai kuwa ni wenye kuzishika amri za Mungu na wenye kungojea Kuja kwa Mwokozi wetu Mara ya Pili katika mawingu ya mbinguni kwa nguvu na utukufu mwingi. Atawaongoza wengi iwezekanavyo kuahirisha siku ya mabaya na kufanana rohoni na walimwengu, wakizifuata desturi za ulimwengu. Nalitishika kuona kuwa roho ya walimwengu ilikuwa ikitawala mioyo na nia za wengi ambao huukiri sana ukweli. Choyo na kutimiza tamaa mbaya bila kujizuia kulipendelewa nao, lakini utauwa halisi na uaminifu safi havikuzwi. 14T 306;KN 95.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents