Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwenye Kuamini-Mtu Bora Katika Biashara

  Mtu mwiminifu kama kilivyo kipimo cha Kristo, ni mtu ambaye ataonyesha uaminifu. Vipimo vya udanganyifu na mizani ya uongo, ambayo kwayo wengi hujaribu kujipatia faida ulimwenguni, ni chukizo machoni pa Mungu. Lakini wengi wanaojidai kuzishika amri za Mungu huvitumia vipimo vya uongo na mizani ya uongo. Mtu akiambatana na Mungu kweli, na akiishika sheria yake kwa kweli, maisha yake yatadhihirisha neno hili; maana matendo yote yatapatana na mafundisho ya Kristo. Hataiuza heshima yake kwa ajili ya pato la faida. Kanuni zinazoyaongoza maisha yake zimejengwa juu ya msingi imara, na mwenendo wake katika mambo ya ulimwengu ni nakili ya kanuni zake. Uaminifu thabiti hung’aa kama dhahabu miongoni mwa mavi ya madini na takataka za ulimwengu.KN 96.3

  Udanganyifu, uongo, na kukosa uaminifu huweza kusetirika na kufichwa machoni pa mwanadamu, lakini si machoni pa Mungu. Malaika za Mungu, wenye kuangalia maendeleo ya tabia na kupima thamani ya tabia ya moyoni, huandika vitabuni mbinguni matendo haya madogo ambayo huidhihirisha tabia. Kama fundi katika kazi za maisha za kila siku si mwaminifu na huidharau kazi yake, walimwengu hawatahukumu isivyo sahihi kama wakikadiria cheo chake katika mambo ya dini kama kilivyo kazini.KN 96.4

  Imani juu ya kukaribia kwa kuja kwa Mwana wa Adamu katika mawingu ya mbinguni haitamfanya Mkristo wa kweli kuwa mtu asiyejali kazi ya kawaida maishani. Wenye kungojea ambao hulitazamia tokeo la Kristo karibuni hawatakuwa wavivu, bali wenye bidii kazini. Kazi yao haitafanywa kwa uzembe na kwa udanganyifu, bali kwa uaminifu, upesi, na kwa ukamilifu. Wale wanaojidanganya kwa kusema kuwa kutojali mambo ya maisha haya ni jambo lionyeshalo hali yao ya kiroho na kujitenga kwao na walimwengu wanadanganyika sana. Kusema kweli kwao, uaminifu, na unyofu hupimwa na kuthibitishwa katika mambo yaliyo ya kitambo tu. Kama ni waaminifu katika lile lililo dogo kabisa watakuwa waminifu katika mengi.KN 97.1

  Nimeonyeshwa kuwa hapa ndipo wengi watashindwa kulistahimili jaribio. Huzikuza tabia zao halisi kwa kuyamudu mambo ya kitambo tu yawapasayo. Hudhihirisha uongo, hila, udanganyifu, katika kushughulika na wanadamu wenzao. Hawafikiri kuwa kupata kwao uzima wa milele kwa wakati ujao hutegemea juu ya namna wanavyoenenda katika maisha haya, na ya kuwa uaminifu mkubwa ni jambo muhimu katika kufanyika tabia ya haki. Kukosa uaminifu ndiyo asili ya hali ya uvuguvugu ya wengi walio umoja na Kristo nao huzidanganya nafsi zao wenyewe. Naona uchungu kusema neno hili kuwa kuna ukosefu wa kutisha wa uaminifu hata miongoni mwa wale waishikao Sabato. 64T 309-311;KN 97.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents