Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Nuru Ilivyomjia Nabii

    Wakati mmoja katika maisha ya wana wa Israeli, kama tulivyokwisha kuona, Bwana aliwaambia watu jinsi apendavyo kuwaletea habari kwa njia ya manabii. Akasema:KN 13.4

    “Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto.” (Hesabu l2:6).KN 13.5

    Katika sura iliyopita umesoma juu ya njozi za Vita Kuu ambazo zilifuatana na mambo fulani ya ajabu yaliyoonekana kwa macho. Pengine mtu aweza kuuliza kwamba kwa nini njozi hizi zilitolewa kwa njia hii? Bila shaka ilikuwa kusudi kuimarisha imani ya watu na kuwahakikishia wote kuwa Mungu alikuwa akisema kwa kweli na nabii huyu. Mara nyingi Ellen White hakusema kwa maneno mengi juu ya hali yake akiwa katika njozi lakini siku moja, alisema, “Ujumbe huu ulitolewa kuthibitisha imani ya wote ili siku hizi za mwisho tuweze kuwa na matumaini katika Roho ya unabii.” Kadiri kazi ya Ellen White ilivyozidi kukua, iliweza kupimwa kwa majaribio ya Biblia kama vile, “Mtawatambua kwa matunda yao.” Lakini inachukua muda matunda kukua na Bwana mwanzo alitoa ushuhuda kwa habari za utoaji wa njozi hii ambayo iliwasaidia watu kuamini.KN 13.6

    Lakini njozi zote hazikutolewa hadharani na kufuatwa na mambo ya kustajabisha ya kuonekana kwa macho. Katika fungu la Biblia mwanzoni mwa sura hii tumeambiwa kuwa siyo kwamba Mungu hujifunua tu kwa nabii “katika maono” bali huweza pia kusema naye “katika ndoto.” Hii ni ndoto ya unabii, kama ile Danieli asemayo habari zake:KN 13.7

    “Katika mwka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo haya.” (Danieli 7:1).KN 14.1

    Kama Danieli asimuliavyo mambo yaliyofunuliwa kwake, mahali kadha wa kadha anasema, “naliona katika maono yangu wakati wa usiku.” Mara nyingi katika maisha ya Ellen White alipewa njozi akili zake zilipokuwa zimeburudika wakati wa saa za usiku. Twasoma mafungu ya maneno ya mwanzoni kama haya. “Katika njozi za usiku nalionyeshwa dhahiri mambo fulani.” au Mungu mara kwa mara amesema na nabii huyu katika ndoto za unabii. Maswali yaweza kuulizwa juu ya uhusiano baina ya ndoto ya unabii au njozi ya usiku, na ndoto ya kawaida. Juu ya nili Ellen White aliandika mnamo mwaka 1868!KN 14.2

    “Ziko ndoto nyingi zinazotokana na mambo ya maisha, ambazo hazihusiani lo lote na Roho ya Mungu. Pia kuna ndoto za uwongo, na maono ya uwongo, ambayo huongozwa na roho ya shetani. Lakini ndoto zitokazo kwa Mungu zimeainishwa katika Neno la Mungu pamoja na njozi. Ndoto za namna hii, tukikumbuka watu walio nazo, na hali ya mambo ambayo kwayo hutolewa, zina uthibitisho wake zenyewe juu ya ukweli wake.”KN 14.3

    Wakati mmoja, baadaye sana katika maisha yake Ellen White, mwanawe, Mchungaji W.C. White, akitaka habari ili kuwasaidia wale wasio na haban, alimwuliza swali hili: “Mama, mara nyingi unasema mambo yaliyofunuliwa kwako saa za usiku. Unasema juu ya ndoto ambazo kwazo nuru hukuzukia. Sisi sote tunazo ndoto. Unajuaje kuwa Mungu anasema nawe katika ndoto ambazo mara nyingi unasema habari zake?”KN 14.4

    Akajibu, “Kwa sababu malaika, mjumbe yule yule husimama karibu nami kuniamuru katika njozi za usiku kama asimamavyo karibu nami akiniamuru katika njozi za mchana.” Malaika anayesemwa habari zake hapa wakati mwingine ametajwa kama malaika,” “kiongozi wangu,” “mkufunzi wangu”, na kadhalika.KN 14.5

    Hapakuwako na matatizo moyoni mwa nabii huyu, wala mashaka yo yote juu ya mafunuo ambayo yalikuja wakati wa saa za usiku; maana hali ya mambo yahusikanayo na mafunuo hayo ilidhihirisha kuwa yalikuwa mafundisho yaliyoamriwa na Mungu.KN 14.6

    Nyakati zingine Ellen White alipokuwa akisali, akisema au akiandika, alipewa njozi. Wale waliomzunguka hawakuweza kufahamu juu ya njozi isipokuwa kama alikoma kidogo ikiwa alikuwa akisema au akisali mbele ya watu. Hivyo siku moja akaandika:KN 14.7

    “Nilipokuwa nikiomba kwa bidii, nilipotewa na kila kitu pande zote kunizunguka; chumba kikajawa na nuru, nami nilikuwa nikisikiliza ujumbe katika mkutano ambao ulionekana kuwa Halmashauri kuu ya Kanisa Ulimwenguni(General Conference).” Miongoni mwa njozi nyingi alizopewa Ellen White katika maisha yake marefu na ya kazi ya miaka 70, njozi iliyokuwa ndefu kuliko zingine ilimchukua saa nne na iliyokuwa fupi ilichukua dakika tu. Mara nyingi zilikuwa kwa nusu saa, au zaidi kidogo. Lakini hakuna kanuni moja iwezayo kutajwa ambayo huzihusu njozi zote, maana ilikuwa kama Paulo alivyoandika:KN 14.8

    “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi.” (Waebrania 1:1).KN 15.1

    Nabii huyu alipewa nuru kwa njia ya njozi, lakini nabii hakuandika akiwa katika njozi. Isipokuwa mara chache, Mungu hakumpa maneno hasa ya kusema. Wala yule malaika hakuuongoza mkono wa nabii katika maneno halisi ya kuandika. Kutoka katika akili zilizotiwa nuru kwa njozi, nabii alisema ama kuandika maneno ambayo yangeweza kupeleka nuru na mafimdisho kwa makutano wake wakiwa wanausoma ujumbe huo au kuusikia ukisemwa.KN 15.2

    Pengine tutauliza, jinsi gani akili za nabii zilitiwa nuru-alipataje habari na maagizo ambayo alipaswa kuyatoa kwa watu? Kama ipasavyo na kanuni moja iwezayo kuwekwa kwa ajili ya kutolewa kwa njozi hizi, Kadhalika ndivyo ipasavyo na kanuni iwezayo kuwekwa kuitawala njia ambayo kwayo nabii alipokea ujumbe kwa kuongozwa na Roho wa Mungu. Lakini, kwa vyo vyote lilikuwa jambo lililo dhahiri ambalo haliondoki akilini mwa nabii. Kadhalika kama mambo tuyaonayo na yanayotupata maishani yanavyokazwa sana akilini mwetu kuliko yale tunayoyasikia tu, ndivyo maono haya kwa manabii, mahali ambapo walielekea kushuhudia kwa macho mambo yaliyobainika, yalivyotia mkazo wa daima akilini mwao.KN 15.3

    Katika sura iliyopita, masimulizi ya njozi ya Vita Kuu aliyatumia maneno yake akielezea jinsi habari za mambo ya historia yalivyomjia. Wakati mwingine akieleza jinsi nuru ilivyomzukia akiwa katika njozi, alisema, “Usikivu wangu mara nyingi ulielekezwa kwenye mambo yaliyobainika duniani. Wakati mwingine napelekwa mbele zaidi katika wakati ujao na kuonyeshwa mambo ambayo hayana budi kuwa. Kisha tena naonyeshwa mambo kama yalivyotukia zamani.”KN 15.4

    Kwa maneno haya inadhihirika kuwa Ellen G. White aliyaona mambo haya yakifanyika, akionekana kama shahidi aliyeyaona kwa macho. Yalitendwa mara ya pili mbele yake katika njozi, hivyo yalikazwa sana akilini mwake.KN 15.5

    Wakati mwingine alijiona kana kwamba alikuwa akiyashiriki mambo aliyoonyeshwa, na ya kwamba aligusa, aliona, akasikia na kutii, hali alikuwa hatendi hivyo kwa kweli, lakini mambo haya yalikazwa akilini mwake kwa namna asivyoweza kuyasahau. Ndivyo ilivyokuwa katika njozi ya kwanza iliyotolewa katika kurasa 34.KN 15.6

    Wakati mwingine akiwa katika njozi, Ellen White alionekana kana kwamba alikuwapo penye mkutano au nyumbani au shuleni mbali. Kujiona kama kweli alikuwa penye mkutano wa namna hii kulizidi hata aliweza kusimulia kwa maneno mengi matendo na maneno yaliyosemwa na watu wengi mbalimbali. Siku moja akiwa katika njozi, Ellen White alijiona kwamba alikuwa amechukuliwa safarini kwenda kwenye hospitali zetu, akizuru vyumba kama ilivyokuwa kawaida, akiona kila kitu kilichokuwa kinatendeka. Juu ya jambo hili akaandika:KN 16.1

    “Mazungumzo yasiyo na maana, maneno ya mzaha, kucheka ovyo, kulisikika kwa uchungu sikioni... Nilishangazwa kuona moyo wa husuda, na kusikia maneno ya wivu, mazungumzo ya kijinga, yaliyopotoka, ambayo yaliwafanya malaika za Mungu kutahayari.”KN 16.2

    Kisha hali zingine za kupendeza za hospitali hiyo hiyo zikafunuliwa. Alipelekwa penye nyumba “mlimotoka sauti ya sala. Sauti hii ilikuwa ya kufurahisha kama nini!” Ujumbe wa mafundisho uliandikwa kutokana na matembezi haya kwenye chuo hiki na juu ya maneno ya yule malaika aliyeonekana kana kwamba alimwongoza katika idara na vyumba mbalimbali.KN 16.3

    Mara nyingi Ellen White alipewa nuru kwa njia ya maono kwa mfano halisi. Maono ya jinsi hii yameelezwa dhahiri katika mafungu manne ya maneno yafuatayo, kutoka kwenye ujumbe uliotumwa kwa mtenda kazi mkubwa aliyeonekana yuko hatarini.KN 16.4

    “Wakati mwingine nilionyeshwa nikikuona katika hali kama ya jemadari, aliyepanda farasi, na kuchukua bendera. Mtu mmoja akaja na kukunyang’anya mkononi mwako bendera hiyo yenye maneno haya “Amri za Mungu na imani ya Yesu,’ nayo ilikanyagwa mavumbini. Nikakuona umezungukwa na watu waliokuungamanisha na walimwengu.”KN 16.5

    Pia palikuwako na nyakati ambapo maono mawili mbalimbali yalionyeshwa kwa Ellen White-moja likieleza jambo ambalo lingetukia kama mipango fulani au sheria fulani zikifuatwa, na katikalingine matokeo ya baadaye ya mipango au sheria zingine. Mfano mzuri wa jambo hili waweza kupatikana kwa habari za kuwekwa kiwanda cha Vyakula vya Afya cha Loma Linda upande wa magharibi ya Marekani. Meneja na wanachama wake walikuwa wakipanga kujenga jumba kubwa karibu sana na jengo kubwa la hospitali. Wakati mipango ilipokuwa ikiendelea, Ellen White nyumbani mwake maili mamia mbali, siku moja usiku akapewa njozi mbili. Juu ya njozi ya kwanza asema:KN 16.6

    “Nilionyeshwa jengo kubwa mahali ambapo vyakula vingi vilitengenezwa. Palikuwa na majengo mengine madogo karibu na mahali pa kuokea mikate. Nikisimama karibu, nilisikia sauti za mashindano juu ya kazi hiyo iliyokuwa ikitendeka. Hapakuwa na masikilizano miongoni mwa watenda kazi, na mashaka yalikuwa yameingia.”KN 16.7

    Kisha akaona meneja aliyesumbuka akijaribu kujadiliana na watenda kazi kuleta maelewano. Akaona wagonjwa waliosikia mashindano haya, na ambao “walisema maneno ya kusikitisha kwamba kiwanda cha chakula kingejengwa juu ya udongo huu mzuri,” karibu sana na hospitali. “Kisha akatokea Mmoja na kusema: Haya yote yamefanywa yatukie mbele yako ili yawe fundisho, kusudi upate kuona matokeo ya kutimiza mipango fulani.”KN 17.1

    Kisha mambo yakabadilika naye akaona Kiwanda cha Vyakula “mbali na majengo ya hospitali, kando ya barabara inayoelekea reli.” Hapo kazi hii iliendeshwa kwa njia ya kujidhili na kupatana na mpango wa Mungu. Katika muda wa saa chache za njozi hii, Ellen White akawa anawaandikia watenda kazi wa Loma Linda, na hili likakata shauri juu ya mahali pa kujengwa Kiwanda cha Vyakula. Kama mpango wao kwanza ungalitimizwa tungeona fadhaa baadaye kuwa na jumba kubwa la biashara karibu na hospitali hii.KN 17.2

    Hivyo yaweza kuonekana kuwa kwa njia nyingi mbalimbali mjumbe wa Mungu alipokea habari na mafundisho kwa njia ya njozi mchana au usiku. Imekuwa kutoka akili zilizotiwa nuru kwamba nabii huyu alisema au kuandika, akipeleka ujumbe wa mafundisho na habari kwa watu. Katika kufanya neno hili Ellen White alisaidiwa na Roho wa Bwana, lakini aliachwa kuchagua maneno ambayo kwayo aweza kuupeleka ujumbe huu. Katika miaka ya mwanzoni mwa kazi yake aliandika katika gazeti la Kanisa letu:KN 17.3

    “Ijapokuwa nategemea msaada wa Roho wa Mungu katika kuandika maono yangu kama nilivyo katika kuyapokea, lakini, maneno ninayotumia katika kuelezea mambo mliyoyaona ni maneno yangu mwenyewe, isipokuwa yakiwa yale niliyoambiwa na malaika ambayo siku zote nayatia katika alama za kunukuu.”KN 17.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents