Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hekima Takatifu Imeahidiwa Kwa Msomaji

    Neno la Mungu, kama tabia ya Mwandishi wake Mtakatifu, hutoa siri ambazo kamwe haziwezi kufahamika kabisa na wanadamu. Huziongoza akili zetu kwa Mwumbaji, ambaye hukaa “katika nuru isiyoweza kukaribiwa.” (l Timotheo 6:16). Hututolea makusudi yake, ambayo yataufikia utimilifu wao tu milele na milele. Hutufanya tuyangalie mafundisho yenye kina kisicho na mwisho na maana kuhusu utawala wa Mungu na hali ulimwenguni.KN 101.2

    Kuingia kwa dhambi ulimwengum, kufanyika mtu halisi kwa Yesu Kristo, kuzaliwa mara ya pili, ufufuo, na mafundisho mengine mengi yaliyotolewa katika Biolia, ni siri kubwa sana kwa akili za mwanadamu kueleza au hata kufahamu kabisa. Lakini Mungu ametupa sisi katika Maandiko Matakatifu mambo ya kutosha kuonyesha utakatifu wao, nasi hatupaswi kuonea mashaka wamekifikia kikomo cha ujuzi na maarifa, wangekoma kuendelea.KN 101.3

    Kama ingewezakana kwa viumbe kupata ufahamu kamili wa Mungu na kazi zake, basi, wakiwa wamekifikia kipeo hiki, pasingekuwako na ugunduzi mwingine tena wa ukweli, wala kukua lcatika kumjua, wala maendeleo mengine ya akili au moyo. Mungu asingekuwa tena Mwenyezi; na wanadamu, wakiwa wamekifikia kikomo cha ujuzi na maarifa, wangekoma kuendelea. Basi, tumshukuru Mungu kuwa hivyo sivyo mambo yalivyo. Mungu hana mwisho; ndani yake yeye kuna “hazina zote za hekima na maarifa.” Na siku zote milele watu watakuwa wakichunguza daima, kuiifunza daima walakini hawawezi kumaliza hazina za hekima yake, wema wake, na uwezo wake.KN 101.4

    Pasipo uongozi wa Roho Mtakatifu tutaelekea daima kuyapotoa Maandiko Matakatifu au kuyafasiri vibaya. Kuna kusoma Biblia kwa namna nyingi ambazo hakuna faida, na mara nyingi ni madhara kwa kweli. Neno la Mungu linapofunuliwa ovyo bila kicho na pasipo kumwomba Mungu, mawazo na upendo wa moyoni visipokazwa kwa Mungu au kupatana na mapenzi yake, moyo utatiwa giza na mashaka; na ye yote anayefungua Biblia na kuisoma kwa njia kama hiyo, moyo wa kuonea mashaka utaimarika. Adui hutawala fikira, na kushauri tafsiri au maana zilizopotoka. 85T 699-705;KN 102.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents