Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kutokuzijua Shuhuda Hizi Si Udhuru

    Wengi wanakwenda kinyume kabisa cha nuru ambayo Mungu amewapa watu wake, kwa sababu hawasomi vitabu vyenye nuru na hekima katika maonyo na makaripio. Masumbufu ya ulimwengu huu, kupenda desturi za walimwengu, na kukosa dini kumewapotosha kutoka katika nuru Mungu aliyotoa kwa neema nyingi, huku vitabu na magazeti yenye makosa vikienda pande zote nchini. Moyo wa kuonea mashaka na ukafiri huzidi kila mahali. Nuru ya thamani kuu itokayo katika kiti cha enzi cha Mungu, imefichwa chini ya kibaba. Mungu atawahesabia watu wake hatia ya kukataa huku. Hesabu haina budi kutolewa kwake kwa kila mwonzi wa nuru kwa maendeleo yetu katika mambo matakatifu, au kukataliwa kwa sababu lilikuwa jambo la kupendeza kuifuata tamaa.KN 109.1

    Shuhuda hizi zingeingizwa kwa kila watu wa nyumbani washikao Sabato, na yawapasa ndugu kujua thamani yao na kuombwa kuzisoma. Haukuwa mpango wa busara sana kuviwekea vitabu hivi hesabu ya chini na kuwa seti moja tu kanisani. Yapasa pawepo katika jamii ya vitabu (maktaba) ya kila watu nyumbani na kusomwa mara kwa mara. Hebu viwekwe mahali viwezapo kusomwa na wengi. 75T 681;KN 109.2

    Nimeonyeshwa kuwa kutokuziamini Shuhuda hizi zenye maonyo, faraja, na laumu hufungia nuru isiwafikie watu wa Mungu. Kutokuamani ni kuyafumba macho yao ili wasiione hali waliyo nayo hasa. Wanadhani ushuhuda wa Roho wa Mungu katika maneno haya ya kukaripia hautakikani au kwamba hauwahusu. Watu kama hao wanaihitaji sana neema ya Mungu na busara ya kiroho, ili wapate kutambua upungufu wao katika ujuzi wa mambo ya kiroho.KN 109.3

    Wengi ambao wameliasi Neno la Mungu hutoa udhuru wa mwenendo wao kuwa hawaziamini Shuhuda hizi. Sasa swali ni hili: Je; wataacha miungu yao ya sanamu ambayo Mungu hukataza, au wataendelea katika upotovu wao wa uzoefu wa anasa na kuikataa nuru waliyopewa na Mungu kugombea mambo yayo hayo wanayojifurahisha nayo? Swali la kujibiwa nao ni hih: Je, nijikane nafsi mwenyewe na kuzipokea shuhuda hizi kama zimetoka kwa Mungu; Shuhuda ambazo hukemea dhambi zangu, au nizikatae Shuhuda hizi kwa sababu zinakemea dhambi zangu? 85T 674, 675;KN 109.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents