Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kufaa kwa Mtu Hutegemea Kujitoa Kwake kwa Roho Mtakatifu

    Mungu hataki tufanye kwa nguvu zetu wenyewe kazi iliyo mbele yetu. Ametujalia msaada wa Mungu kwa hatari zote ambazo hushinda njia za wanadamu. Hutoa Roho Mtakatifu kusaidia katika kila shida, kutia nguvu matumaini yetu, kutia nuru akili zetu za moyoni na kuisafisha mioyo yetu.KN 114.3

    Kristo amefanya matayarisho ili kanisa lake liwe jamii ya watu walioongoka, ambao wameangazwa na nuru ya mbinguni, wenye utukufu wa Imanueli. Ni kusudi lake (Kristo) kwamba kila Mkristo awe amezungukwa na hali ya kiroho ya nuru na amani. Hakuna kikomo cha hali ya kufaa ya mtu ambaye, huweka kando moyo wa choyo au kujifikiri nafsi mwenyewe, na kutoa nafasi kwa kazi ya Roho Mtakatifu moyoni mwake na kuishi maisha ya kujitoa wakfu kabisa kwa Mungu.KN 114.4

    Matokeo ya baadaye ya kumwagiwa Roho ile siku ya Pentekoste yalikuwa nini? Habari njema za furaha ya Mwokozi aliyefufuka katika wafu zilienezwa hata miisho ya ulimwengu uliokaliwa na watu (zamani zile). Mioyo ya wale wanafunzi ililemewa na mzigo wa ukarimu mwingi, wenye kina, na wenye kuenea sana ambao uliwahimiza kwenda hata mwisho wa nchi wakishuhudia na kusema: “Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.” (Wagatia 6:14). Kadiri walivyolihubiri neno la kweli jinsi lilivyo ndani ya Yesu, mioyo ilishindwa na uwezo wa ujumbe huu. Kanisa likaona waongofu wakilijia kwa wingi kutoka pande zote. Watu walioasi dini wakaongoka tena. Wenye dhambi wakaiiunga na Wakristo katika kuitafuta lulu ya thamani kuu. Wale ambao walikuwa adui wakali kabisa walioipinga Injili wakawa ndio wenye kuitetea kwa ujasiri. Unabii ukatimizwa: Yeye aliye dhaifu atakuwa “kama Daudi.” Nayo nyumba ya Daudi itakuwa “kama malaika wa Bwana.” Kila Mkristo aliona ndani ya ndugu yake mfano mtakatifu wa upendo na moyo wa ukarimu. Moyo mmoja ulienea kwa wote. Jambo moja la moyo wa bidii lilimeza mengine yote. Tamaa tu ya waaminio ikiwa kuonyesha tabia ya Kristo jinsi ilivyo na kufanya kazi kuueneza ufalme wake.KN 114.5

    Kwetu leo, kama ilivyokuwa kwa wale wanafunzi wa kwanza, tunayo ile ahadi ya Roho. Mungu leo atawajalia wanaume Siku ya Pentekoste walisikie Neno la wokovu. Saa hii hii Roho wake na neema yake ni kwa wote wanaozihitaji na watakaoliamini Neno lake. 38T 19, 20;KN 115.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents