Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Roho Mtakatifu Atakaa hata Mwisho

    Kristo alisema kuwa mvuto mtakatifu wa Roho hauna budi kukaa na wafuasi wake hata mwisho. Lakini ahadi hii haithaminiwi kama ipasavyo; na kwa hiyo kutimizwa kwake hakuonekani kama ambavyo ingalikuwa. Ahadi ya Roho ni neno lisilofikiriwa sana na matokeo ya baadaye huwa yale tu yawezayo kutazamiwa-kukosa mvua ya kiroho, giza la kiroho, upungufu wa kiroho, na mauti. Mambo madogo yasiyo na maana hushika usikivu wa watu, na uwezo mtakatifu ambao unalazimu kwa maendeleo na mafanikio ya kanisa, na ambao ungeleta mibaraka yote mingine pamoja nao, unakosekana, ingawa umetolewa kwa wingi kabisa.KN 115.2

    Utovu wa Roho ndio ufanyao kazi ya Injili isiwe na nguvu. Elimu, talanta, ufasaha wa maneno, kila kipawa cha asili au cha kujipatia, huweza kupatikana lakini, pasipo Roho wa Mungu, hakuna moyo utakaoguswa, wala mwenye dhambi atakayeongolewa kwa Kristo. Ambapo, kama wakiwa na umoja na Kristo kama wanazo karama za Rono, maskini kabisa na wajinga sana miongoni mwa wanafunzi wake watakuwa na uwezo ambao matokeo yake yataonekana mioyoni. Mungu huwafanya njia ya mafuriko ya mvuto bora kabisa ulimwenguni.KN 115.3

    Moyo wa bidii kwa Mungu uliwasukuma wale wanafunzi kulishuhudia Neno la Mungu kwa nguvu. Je, haipasi moyo huu kuwaka mioyoni mwetu tukikusudia kusimulia habari za upendo uokoao, za Kristo aliyesulibiwa? Je, haipasi Roho wa Mungu kufika leo, kwa kujibiwa sala iliyoombwa kwa bidii, na kuwajaza watu uwezo wa kufanya kazi? Kwa nini, basi kanisa ni dhaifu sana na lisilo na Roho? 48T 21, 22;KN 115.4

    Roho Mtakatifu akitawala mioyo ya washiriki wetu wa kanisa, itaonekana makanisani mwetu hali ya juu zaidi katika mazungumzo katika kazi, katika mambo ya kiroho, kuliko inavyoonekana sasa. Washiriki wa kanisa wataburudishwa na maji ya uzima, na watenda kazi wafanyao kazi chini ya Bwana mmoja, yaani Kristo, watamdhihirisha Bwana wao katika roho, katika neno, katika tendo, na wataiona nguvu kuonga mbele katika ongezeko la nguvu la umoja na upendo, ambao utatoa ushuhuda kwa walimwengu kwamba Mungu alimtuma Mwanawe kufa kwa ajili ya wokovu wa wenye dhambi. Neno takatifu la kweli litatukuzwa; na kadiri ling’aavyo kama taa iwakayo tutalifahamu wazi zaidi. 58T 211; KN 115.5

    Nalionyeshwa kuwa kama watu wa Mungu hawajibiidishi, ila kungojea tu kuburudishwa kuwafikie na kuondoa mabaya yao na kuwatoa makosa; kama wakitegemea hilo kuwasafisha na uchafu, kilio cha sauti kuu ya malaika wa tatu, wataonekana wamepungua. Kuburudishwa au uwezo wa Mungu huja tu juu ya wale ambao huwaagiza kufanya, yaani, kujitakasa narsi zao na uchafu wote wa mwili na roho, wakitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. 61T 619.KN 116.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents