Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Njia Kuu ya Shetana ya Kuleta Uharibifu

    Shetani aliwakusanya malaika wabaya pamoja kutafuta njia ya kufanya uovu mkubwa iwezekanavyo kwa wanadamu. Mashauri yakatolewa moja moja, mpaka mwishowe Shetani mwenyewe akafikiri njia. Akapenda kuyatwaa matunda ya mzabibu, pia ngano, na vitu vingine vilivyotolewa na Mungu chakula, na kuvigeuza viwe sumu ambayo ingeuharibu uwezo wa mwanadamu wa mwili, akili, na tabia ya moyoni, na hivyo atazishinda akili za kupambanua mema na mabaya hata Shetani apate kutawala kabisa. Kwa mvuto wa pombe watu huweza kufanya makosa ya uhalifu wa sheria ya kila namna. Kwa njia ya tamaa ya chakula iliyopotoka, walimwengu huharibiwa. Kwa kuwaongoza kunywa kileo, Shetani huweza kuwafanya wazidi kupungua kwenye mizani. 4Te. 12;KN 117.5

    Shetani anauteka ulimwengu nyara kwa njia ya kutumia pombe na tumbaku, majani va chai na kahawa. Akili Mungu alizotoa, ambazo zapaswa kuwekwa safi bila kizuizi, hupotoshwa kwa kutumia vitu vinavyozimua nguvu mwilini. Ubongo hauwezi tena kupambanua vizuri mema na mabaya. Adui hutawaia. Mwanadamu ameuza akili zake kwa kile ambacho humfanya kuwa mwenye wazimu. Hajui kitu kilicho halali. 5Ev. 529;KN 118.1

    Mwumbaji wetu amemjalia mwanadamu mengi kwa ukarimu. Kama majaliwa haya yote ya Mungu yangetumiwa kwa busara na kwa kiasi, umaskini, ugonjwa, na dhiki vingekuwa karibu sana kuondolewa mbali kutoka duniani. Lakini ole, twaona pande zote mibaraka ya Mungu ikabadilishwa kuwa laana kwa uovu wa wanadamu.KN 118.2

    Hakuna watu wenye hatia ya upotovu na wenye kutumia vibaya vipaji vya Mungu vya thamani kuliko wale ambao huyatumia mazao ya udongo katika kutengeneza pombe. Nafaka za chakula, matunda matamu, hugeuzwa kuwa vinywaji ambavyo huzipotosha na kuzirusha akili. Kama matokeo ya kutumia sumu hizi maelfu ya watu nyumbani hukosa raha na hata riziki zenyewe za maisha, mauaji na uhalifu wa sheria huzidi, na magonjwa na mauti huwaharakisha maelfu ya wenye kuvitumia vitu hivi kwenye kaburi la mlevi. 6GW 385, 386;KN 118.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents